Wazo: Ianzishwe kampeni changia Lissu kadri anavyokaa mahabusu

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Inabidi tujiongeza kwa kuonyesha tuko pamoja na Lissu kwa kuanzisha kampeni maalumu ya kumchangia ambayo itakoma pale tu siku anapopewa dhamana.

Fedha zitakazopatikana zielekezwe katika kutatua matatizo yaliyoko katika jimbo lake kwani watu wa jimbo hilo ndio waliotuletea mpambanaji huyu.

Wakati wao wanamshikilia,sisi tunamuwezesha.

Nina hakika michango hiyo itaandika historia na itawashitua wale jamaa.

Akikaa ndani miezi kama Lema basi atoke na mamilioni kadhaa.

Wekeni utaratibu wa wazi watu kuchangia muone muitikio wake.

Kuna watu wanatuhumiwa kununua madiwani na wengine kutoa mikopo kwa vijana hivyo sioni tatizo na sisi tukaja na huu mkakati.

Tjifunze kwa yaliyomkuta Lema na tuwe na mkakati wa ku-discourage haya mambo.
 
Kwa nini tusimchangie mtoto wa Ben Saanane?? Maana hadi sasa imebaki story..na chama hakitaki tena hata kuzungumzia..ila kumtukana Kiongozi wa nchi ndio nyepesi zaidi kwao kuliko kumzungumzia Saanane
 
Haukuwahi kuwaza kitu kama hiki toka kiongozi kijana mwandamizi wa chama fulani cha siasa aache kutweet!
 
Back
Top Bottom