Waziri wa Zimbabwe adai upinzani una njama ya kuingiza silaha nchini

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,033
9,923
Emmerson Mnangagwa


Waziri wa usalama wa kitaifa wa Zimbabwe, Owen Ncube, anadai kuwa upinzani unafanya kazi na nchi za magharibi kuingiza silaha kimagendo nchini humo kwa lengo la kumuondoa madarakani Emmerson Mnangagwa.

Maafisa kutoka chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change hata hivyo wamepuuza madai hayo wakisema kuwa hayana msingi wowote.

Bila kutoa ushahidi, Bw. Ncube amesema nchi za Magharibi ambazo hakuzitaja zimekuja na mkakati wa kuvuruga utawala wa Zimbabwe ili wathibitisha haja mataifa ya kigeni kuingilia kati kutatua mzozo.

Makundi ya kutetea haki yanasema serikali ya Rais Mnangagwa imekuwa ikikosolewa vikali hasa wakati huu ambapo mzozo wa kiuchumi ya nchi hiyo unaendelea kufukuta.

Wamelaani hatua ya hivi karibuni ya kufungwa kwa wanasiasa na wanaharakati kwa kile walichodai kuwa mashitaka ya uwongo.
 
Back
Top Bottom