Waziri wa Viwanda: Tumeongeza kodi kwenye mitumba na itapigwa marufuku ndani ya miaka mitatu

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968



Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage amesema hawana dhamira ya kuwafanya watanzania watembee uchi, na kwamba wamepandisha kodi kwenye nguo za mitumba ili wenye viwanda vya ndani wazalishe kwa wingi zaidi na ndani ya miaka mitatu mitumba itapigwa marufuku na kuwataka wananchi na wadau wa biashara na viwanda kutowaombea watanzania ili waendelee kuvaa mitumba
 
Tatizo viwanda vyenyewe havizalishi qaulity nzuri.Ukipata nguo au raba ya mtumba ya elfu 35 inakuwa kali sana kuliko hata hiyo product mpy ya KTM au NIDA .
Wangesema tu kuwa grade fulani ya mtumba hatuihitaji ila zile first grade wangeruhusu tu ziingie.
 
Sasa ukisikia maamuzi ya kukurupuka ya serikali ya awamu ya 5, basi ni haya ya design hii.

Sisi wananchi masikini tumekuwa kwa miaka mingi tikiponea kwenye mavazi ya mitumba.

Wala huyo Waziri wa viwanda asitake kuudanganya Umma wa watanzania kuwa within 3 years nchi itakuwa na viwanda vya nguo vya kuwavalisha watu milioni 45!

Pia ni dhahiri kwa mwendo huu wa serikali ya awamu ya 5 kufikia azma ya nchi ya viwanda ni sawasawa na 'daydream'

Inawezekana sasa serikali ya awamu ya 5 inataka kutimiza azma yao kubwa iliyojificha 'under the carpet' za kutaka kila mtu aishi kama shetani, na watanzania kwa mamilioni waanze kutembea uchi mabarabarani....

Naweza kudiriki kuiita hiyo kauli ya kuwa within 3 years kutapigwa marufuku ya kuingiza nguo za aina yote ya mitumba kuwa ni mawazo purely ya kishetani!
 
Akili za Mwendo kasiii..
Kilasafarii inawezekana..
Raha sana kuskia haya matamko yakutukuza mfalme..
 
Ningekuwa mimi waziri hizo nazo ningepandisha bei kwa kuzipiga kodi. Hivi kweli Watanzania tunashindwa kushona nguo? Mbona zamani tulikuwa tunashona?
Ndiyo maana wewe hujawa waziri, kwasababu weww waapenda nguo za kushona hivyo kila mtu avae za kushona? Huo ni umimi...ni ugonjwa mbaya sana...utazuia watu wasivae suti au kanzu kisa wewe unajifunga lubega au zamani tukijifunga lubega!!!
 
Ningekuwa mimi waziri hizo nazo ningepandisha bei kwa kuzipiga kodi. Hivi kweli Watanzania tunashindwa kushona nguo? Mbona zamani tulikuwa tunashona?

tunaweza kushona nguo zetu ila maendeleo ya teknohama dunia imekua kijiji tunataka kwenda na fashion za duniani huko

sasa viwanda vya ndani vinajaribu kwenda na fashion ila ndio poor quality na bei juu, mitumba bei afadhali na quality nzuri. China ndugu zetu quality ni kipato na preference zako tu.

ni wazo zuri ila liwe na mikakati thabit na serikali isapoti na kuweka angalizo kwa viwanda vya ndani na kuvuti wawekezaji wa nje na ndani ktk sekta ya nguo
 
Sasa ndiyo napata tafsiri kwa nini serikali ya awamu ya 5 imeamua kutotaka mawazo mbadala ndani ya Bunge na nje ya Bunge, kwa kuwa wanajua ideas za 'kichizi' za dizaini hiyo hata mtoto anayesoma chekechea atayapinga.

Hivi huyo Waziri wa viwanda anataka kuturejesha maisha kama waliyokuwa wakiishi wachina miaka ile ya 70 ambapo Taifa zima la wachina walikuwa wakivalishwa uniforms ambazo ni za khaki ambazo ni brand new ambazo tayari wameshazibandika viraka?!

Huu 'wehu' wa viongozi wetu ifike mahali sasa sisi watanzania tuwaambie FULL STOP.......
 
Back
Top Bottom