MP CHACHANDU
JF-Expert Member
- Dec 4, 2016
- 875
- 616
Amesema swala La ajira kwa vijana ni changamoto kubwa ambayo haina ufumbuzi amesema ameifananisha na damu changa ambayo haigusiki hata kigodo.
======
Waziri kuita damu changa ajira
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amesema anakusudia kubadilisha uongozi wa juu wa Shirika la Posta kwa kuwaweka vijana ili lijiendeshe kiuchumi.
PROFESA MAKAME MBARAWA.
Aidha, ameiagiza Bodi ya shirika hilo kuchukua hatua dhidi ya `madudu' yaliyobainika mikoani ya kulihujumu shirika hilo.
Prof. Mbarawa aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana alipofanya ziara ya kukagua utendaji kazi wa shirika hilo pamoja na kuzungumza na wafanyakazi.
Alisema katika ziara aliyoifanya kuzungukia Shirika la Posta nchini, amebaini changamoto kubwa ya uongozi unaosababisha kudumaa kwa shirika na si tatizo la fedha.
Alisema kuna haja ya kuwapo kwa uongozi imara ambao utalivusha shirika kwa kuwa lina rasilimali nyingi za kutosha katika kujiendesha kiuchumi.
“Shirika la Posta lina uwezo mkubwa, lakini bado hawautumia. Hawajapata viongozi wa kulisimamia, mwanzo kulikuwa na mgogoro kwenye Shirika la Reli (TRL) kila siku mara migomo, tukajiuliza dawa ni nini ni pesa au.. tukagundua pesa hazitamaliza matatizo, dawa ni kupeleka uongozi mpya.
Tumempeleka kijana, sasa mambo yanakwenda vizuri hata wafanyakazi hatuwasikii wakilalamika ni kwa sababu amepatikana kiongozi mzuri. Na hapa nitamtafuta kijana mmoja makini na atalibadilisha shirika hili na kuonekana lipo jipya,” alisema.
"Hili shirika ni tajiri, lina nyumba nyingi, nimeambiwa na Mwenyekiti wa Bodi kuwa walikwenda Makambako wakamkuta mtu amejenga nyumba kwenye kiwanja cha Posta. Hata viongozi wa Posta wenyewe hawajui, hii ni biashara gani? Mmefanya kama shamba la bibi kila mtu anapiga… kuna nyumba zenu Kisutu mmepangisha, lakini hakuna kitu,” alisema Prof. Mbarawa.
Waziri Mbarawa aliwataka wafanyakazi hao kuhakikisha wanasimamia vyema rasilimali za Posta.
“Ukiniambia kuhusu fedha mimi siwezi kuleta fedha, ni heri nikawa mkweli. Kwanza mna fedha eti leo naambiwa natakiwa nilete Sh. bilioni 19! Hayo mambo msiniambie. Fedha mnazo, mna maghorofa, kwa nini hamfanyi kazi? Posta nzima nimekuta wateja 20! Hamuoni aibu? Mnakaa mnafanya nini? Hamuendi kujitangaza, kutafuta wateja. Hivi Posta kubwa kama hii hakuna wateja? Alihoji Prof. Mbarawa.
Aidha, alisema Bodi imewasilisha ripoti ya mambo mengi yaliyofanyika mikoani, hivyo lazima hatua zichukuliwe.
Wafanyakazi hao walilalamikia suala la uongozi mbovu, kutokuwapo kwa ushirikiano baina ya wafanyakazi na menejementi, maslahi ya mshahara na kukosekana kwa magari ya kusafirisha mizigo mkoani, hali waliyosema hulilazimu shirika kulipa gharama kubwa kwa magari ya kukodi.
Chanzo: Nipashe