Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
View attachment 845756
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Selemani Jafo, akiwa anaongea kwenye kipindi cha Tunatekeleza cha TBC, saa 6 mchana, amesifia kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuibadilisha Tanzania kuelekea katika uchumi wa kati na kwamba kwa kasi hiyo, "Watu watakuja kujifunza juu ya utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano."
Jafo alitoa takwimu kadhaa zinazoonyesha mabadiliko makubwa yaliyofanywa ndani ya kipindi kifupi tangu Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Rais Dk. John Pombe Magufuli iingie madarakani mwaka 2015. Baadhi ya mambo aliyoongelea kwenye sekta za Afya na Elimu ni yafuatayo:
Waziri aliwakumbusha Wakurugenzi wa Halmashauri juu ya wajibu wao katika kuharakisha maendeleo kwenye maeneo yao na "kuwaonya Wakurugenzi wasioendana na kasi ya Serikali wasione ajabu wakiondolewa kwenye nafasi zao na wasitafute mchawi kuwa, sijui wamerogwa bali ni utendaji kazi wao."
Jafo alidai kuondolewa kwa Wakurugenzi Watendaji wa Kigoma Mjini, Pangani na Nkasi ni kutokana na kutoendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Jafo akiwa kwenye Kikao na Wadau wa Elimu nchini jijini Mwanza, mwaka 2017, alitabiri mabadiliko makubwa katika performance ya shule za Serikali kulinganisha na za binafsi kwa sababu ya maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali kwa shule zake, ikiwemo kujenga maabara za sayansi, kuondoa ada, kusambaza vitabu, kutengeneza madawati, kuongeza vyumba vya madarasa na kuajiri walimu wengi mpaka kufikia mahitaji ya walimu wa Arts kutosheleza kabisa. Aliwaambia wadau kuwa, ana uhakika ni shule chache tu za binafsi zitabakia kutokana na maboresho hayo makubwa yakiwemo ya kukarabati shule kongwe. Matokeo ya Kidato cha VI mwaka 2018, ni mwanzo tu wa "changing of guard" kati ya shule za umma dhidi ya za binafsi.
Mnyonge mnyongeni haki yake mwachie. Iliyokwishayafanya ni mengi mno kwenye sekta ya elimu na afya, wote tunaona.

- Sekta ya Afya: Tangu Tanzania ipate uhuru mwaka 1961 hadi mwaka 2015, kulikuwepo Vituo vya Afya 515, kati ya hivyo, vinavyotoa huduma za upasuaji 115 pekee lakini ndani ya miaka miwili na nusu, Vituo vya huduma ya upasuaji vimeongezeka na kufikia 204, sawa na ujenzi wa vituo 89 ndani ya miaka miwili pekee. Alisema kuwa, wakati Serikali ya Awamu ya Tano inaingia madarakani, kulikuwepo hospitali 72 pekee katika jumla ya Halmashauri 184 nchini lakini ndani ya Bajeti ya mwaka huu wa 2018/2019 pekee, Serikali itajenga hospitali 63 huku Vituo vya afya 67 vikiwa vinajengwa Nchi nzima.
- Elimu Msingi Bila Malipo: Kumekuwepo kasi kubwa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, maabara na madawati kwa ajili ya kukidhi ongezeko kubwa la wanafunzi. Alitolea mfano wa Shule ya Msingi Maji Matitu, jijini Dar es Salaam, iliyokuwa imepanga mwaka 2017 kusajili (maotea) wanafunzi 260 lakini ilijikuta ikisajili wanafunzi 1026!! Vilevile, upatikanaji wa vitabu umeongezeka kutoka wanafunzi 8 kwa kitabu hadi wanafunzi 3 kwa kitabu.