Waziri wa sasa wa nishati anafeli wapi kuhusu suala la kutokatika umeme kahama?

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Nakumbuka kipindi cha prof muhongo tulipumzika kidogo na hii kadhia ya kukatika kwa umeme.
Sasa umeme kahama hautabiriki kabisa.Utakatika kila jumapili.Utakatika muda wowote kutwa nzima.Na sasa niandikapo umekatika.
Huyu waziri amekwama wapi?
Maana isije kuwa hujuma ya wauza mchele.Maana umeme ukikatika hivi,mchele unapanda bei.
Kibaya zaidi hawatoi taarifa.Hivi mnasubiri hadi Rais aje kuwaelekeza nini cha kufanya?
Unafeli wapi mheshimiwa waziri kuwasimamia watu wa kahama.Maana naona wanafanya kazi kwa mazoea
 
Mnyonge mnyongeni lkn haki yake mpeni, nikweli kuna laini umeme umekua ukikatika mara kwa mara lkn kwenye swala la matangazo na kutoa taarifa wamekua wakijitahidi sana mfano hili katizo la j.pili ya leo jana majira ya saa 2 usiku walipita wakitangaza mitaa ya nyakato, pia wana group la whatsup ambako nimeshuhudia wakitoa taarifa zao mara kwa mara.

Nadhani ukiwafuatilia kwa ukaribu utaona jitihadazao.
 
Back
Top Bottom