si waongee na BIGSHOW aruhusu gas ya mtwara chapchap.Kigamboni ulikatika saa tano asubuhi na umerudi saa sita usiku, tumepiga Tanesco wamesema kuna upungufu wa uzalishaji wa Gas.
Ndugu wanajf nimekuwa nikifuatulia kwa karibu sana jinsi waziri wa nishati prof. muhongo anapolidangaya taifa letu kuwa hakuna mgao wa umeme. Je anafanya hivyo kwa maslahi ya nani wakati nchi ipo gizani? Leo nimefuatilia na kugundua kuwa zaidi ya mikoa kumi haina umeme. Hivi huyu ni prof kweli au ni prof kama vile wale wanaojiita hivyo? Namuomba aache mara moja kulidanganya taifa maana ulimwengu wa sasa si kama wa miaka ya arobaini na saba aliyozaliwa yeye! Kama ataendelea na uongo wake wanajf tuitishe maandamano ya kudai umeme na pia kumtaka waziri muhongo achie ofisi ya umma maana bado hatujafikia kuongozwa na waziri muongo.
Labda nikuambie kwa kifupi ndugu yangu nchi hii imekwama na kupoteza mvuto,mambo yanajiendea yenyewe hakuna anayejali watu wanajifanyia wanayoyajua wao na hii inatokana na Viongozi na watendaji wa taifa kutojali maslahi ya nchi na kujali yao binafsi maana haiwezekani wale maadui wakubwa ambao muasisi wa taifa hili J.K NYERERE aliwapigia kelele miaka zaidi ya hamsini mpaka leo hata mmoja hajaondolewa,angalia Elimu matokeo zero tupu huo ujinga tunaotaka kuutokomeza ndio huu,Umaskini huu ndio sitaki hata kuuongelea,Maradhi na hili liko wazi kwani haya yote matatu yanaenda pamoja,Kwa kifupi hii nchi ina allergy na maendeleo kwani mtu akitaka kuleta maendeleo tu nchi inapiga chafya,fanya mambo yako tu.......Ndugu wanajf nimekuwa nikifuatulia kwa karibu sana jinsi waziri wa nishati prof. Muhongo anapolidangaya taifa letu kuwa hakuna mgao wa umeme. Je anafanya hivyo kwa maslahi ya nani wakati nchi ipo gizani?
Leo nimefuatilia na kugundua kuwa zaidi ya mikoa kumi haina umeme. Hivi huyu ni prof kweli au ni prof kama vile wale wanaojiita hivyo? Namuomba aache mara moja kulidanganya taifa maana ulimwengu wa sasa si kama wa miaka ya arobaini na saba aliyozaliwa yeye!
Kama ataendelea na uongo wake wanajf tuitishe maandamano ya kudai umeme na pia kumtaka waziri Muhongo achie ofisi ya umma maana bado hatujafikia kuongozwa na waziri muongo.
Labda nikuambie kwa kifupi ndugu yangu nchi hii imekwama na kupoteza mvuto,mambo yanajiendea yenyewe hakuna anayejali watu wanajifanyia wanayoyajua wao na hii inatokana na Viongozi na watendaji wa taifa kutojali maslahi ya nchi na kujali yao binafsi maana haiwezekani wale maadui wakubwa ambao muasisi wa taifa hili J.K NYERERE aliwapigia kelele miaka zaidi ya hamsini mpaka leo hata mmoja hajaondolewa,angalia Elimu matokeo zero tupu huo ujinga tunaotaka kuutokomeza ndio huu,Umaskini huu ndio sitaki hata kuuongelea,Maradhi na hili liko wazi kwani haya yote matatu yanaenda pamoja,Kwa kifupi hii nchi ina allergy na maendeleo kwani mtu akitaka kuleta maendeleo tu nchi inapiga chafya,fanya mambo yako tu.......
Charambe na chamazi huko mbagala hakuna umeme toka asubuhi hadi sasa
Elimu ambayo haina msaada kwa taifa hata kama ni uprofesa haina maana yoyote,kwani kwanini tunasoma?nchi hii ina sarakasi nyingi sana,KAMA SI MGAO TATIZO LA UMEME LA SASA LIMETOKANA NA NINI WE PROFESA?Ndugu zangu, achaneni na wasomi wa ovyo kama huyu Prof.Muongo kama jina lake lilivyo.Kuna Mgawo wa juu sana katika jiji la Dar.Kila siku kuna mgawo wa zaidi ya masaa matano.Mimi naishi Magomeni Mikumi leo hii 28/2/2013 umeme umekatika 12asubuhi na mpaka sasa hakuna umeme.Na nik awaida kukatika kuanzia 12jioni na kurudisha saa tano usiku au kukata saa tano asubuhi na kurudisha jioni 12.Kwa hiyo Prof Muongo ni bonge tu la tapeli la kisiasa na kisomi lililetwa na baba lao.Kumbukeni kawaida ni mtoto wa nyoka ni nyoka na kama baba kama mtoto.Nilimsikia juzi RadioOne anaongopa tu eti kuna matengenezo ,kwani yanafanyika na usiku, hayaishi,na kwa sehemu kiasi gani?.shame to u TANESO and ur crook Prof.
Naheshimu jina lako Nsabhi. lakini kwa maoni yako ya maandamano nahisi umetumwa na wanasiasa. acheni siasa tufanye kazi tusonge mbele ww unadhani kwa hali shirika alilivyolikuta huo umeme atoe nyumbani kwake akuletee. Badala ya kupigania mfumo ubadilike siasa isitawale kila sector wewe unapigana na wazir. for ur info hujamfuatilia kwa karibu Prof kama unavyotueleza hapa hayo ni majungu tu. Prof ana projects nyingi sana na akipata fungu utamsifia kama huyo alieukana u-TZ na kwenda ka-nchi ambako naamini kagame akitoka tu wananyukana tena. tufanye kazi , tuache siasa, tuache kuwa vibaraka wawanasiasa na tuache majungu.