Waziri wa Nishati aagiza kuondolewa kwenye nafasi yake, Meneja wa REA Morogoro

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amemuagiza Mkurugenzi wa miradi ya Umeme Vijijini (REA) kumuondoa kwenye nafasi ya Umeneja wa REA Mkoani Morogoro, Seif Abdallah

Waziri amesema Meneja huyo ameshindwa kumsimamia mkandarasi kikamilifu anayesambaza umeme Mkoani humo kwani ujenzi wa miundombinu upo kwa 56.6% huku katika mikoa mingine ukiwa kwa 70%

Akiwa katika uzinduzi wa umeme huo katika vijiji vya Makanga na Idunda Wilayani Ulanga, Waziri Kalemani amesema “Meneja wa REA wa Mkoa huu, yupo wapi? Anayemsimamia mkandarasi yupo wapi? Mimi nipo hapa yeye yupo wapi?”

Ameongeza “Nimepiga simu nimeambiwa hayupo, jana pia hakuwepo. Mimi Waziri nipo yeye yupo wapi? Sasa naagiza DG (Director General) wa REA amuondolee Umeneja leo leo.”
 
Back
Top Bottom