Waziri wa mambo ya ndani nchi ina wakimbizi wa ndani sina uhakika kama hili unalijua

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
May 11, 2015
23,372
54,931
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI NCHI INA WAKIMBIZI WA NDANI SINA UHAKIKA KAMA HILI UNALIJUA.

Salaam kwako waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mh.Mwigulu Lameck Nchemba pamoja na watanzania wote kiujumla, naandika waraka huu kwako na kwa umma wa watanzania kukueleza yale yaliyopo ndani ya nchi japo yamefichwa (hayaonekani).

Waraka huu una mengi sana ya kujiuliza ni vipi serikali itasaidia hawa wakimbizi ambao sasa wapo nchini tena wakimbizi ndani ya nchi yao (samahani sana kwa kutumia neno WAKIMBIZI ila naomba nivae uhalisia uliopo ili kunusuru watu hawa).

Sifa za mkoa wa Mara zimekuwa zikijulikana moja kwa moja na kwa hali ilivyo sasa hivi ukweli ni kwamba vitendo vinavyofanyika mkoani Mara ni vya ajabu na vinatia aibu Taifa la Tanzania ndani ya mipaka yetu na nje ya mipaka.

Sio neno geni masikioni mwako Mh ukisikia neon UKEKETAJI, najua ni neno ambalo sasa hivi hapa nchini linazoeleka masikioni mwetu ,Licha ya Makabila baadhi hapa nchini kufanya kitendo hicho kwa wanawake bado nguvu kubwa haijaelekezwa ili kupambana na vitendo hivi vya udhalilishaji kwa mtoto wa kike, hata kama kuna jitihada ila naomba ziongezwe mara 5 zaidi ya sasa, (naomba sasa nikupe kiini).

Kwenye wilaya ya Tarime mkoani Mara kuna mamia ya watoto wa kike walikimbia ukeketaji na kuhifadhiwa na ATFG-MASANGA. (ASSOCIATION FOR TEMINATION OF FEMALE GENITAL MULTILATIONS) watoto hawa walifika kwenye kambi hiyo tarehe 22.09.2016 na kambi hiyo ikafungwa mwaka huu ili watoto warudi nyumbani na kurejea masomoni 03.01.2017.

Ndugu Watanzania cha achabu na cha kusikitisha hadi sasa hapo kambini kuna wototo wapatao 70 ambao wamekataliwa na wazazi wao baada ya kutoroka majumbani kwao kisa UKEKETAJI na cha kusikitisha zaidi wazazi wanataka mabinti hao wakeketwe ndipo watawatambua kama watoto wao.

Hiyo moja,Pili kuna mmoja ambae yeye alishindwa kabisa kuvumilia na akakubali kufanyiwa kitendo hicho ndipo alipokelewa na wazazi wake (inauma sana), watoto hawa wengi wao ni wanafunzi na shule zimefunguliwa tafadhali Mh.hebu waone huruma watoto hawa namna gani ya kuwasaidia ili waendelee na masomo yao.

Sitakuwa na furaha mimi kama mtanzania nikiishi kwa furaha huku wenzangu tena watoto ambao tunawatengeneza kuwa warithi wetu wakikaa kambini ile hali wana wazazi na wanapajua nyumbani. Hebu tusimame wima kutetea hawa watoto wadogo ambao wengi hawajatimiza ndoto zao na wanahitaji kutimiza ndoto hizo kwa kupata elimu.

Waziri Mwigulu naomba vaa vazi lako usaidie hawa watoto, najua mtoto ni ngumu kusahau na msaada wako kwao ni kumbukumbu tosha maishani mwao hawatasahau pale utakapowatoa huko kambini na kuwarejesha makwao na kuendelea na maisha yao kama awali.

MWISHO KABISA; Naamini usikivu wako utasaidia hawa watoto kurudi makwao na kuanza masomo yao na hivi vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia hasa ukeketaji naomba hatua kali za kisheria zichukuliwe ili kunusuru watoto hawa (naanza kupata picha halisi nini chanzo cha watoto wa mitaani).

(Nimeshindwa kuweka sauti zao hapa)
KILA LA KHERI KATIKA UTATUZI WA HILI
 
Back
Top Bottom