Wanajopo mimi nimeona nilete hii mada ili tuichangie,kwani kila wakati hapa nchini kunatokea vurugu za wananchi kuandamana kwa kulalamikia utendaji kazi wa Jeshi la Polisi lakini hawa viongozi wapo tu kimya hawatoi matamko yoyote,hali ambayo yamesababisha hasira kwa wananchi kulipa kisasi kwa kuvamia vituo vya Polisi,wananchi wanauwawa na Polisi lakini hawa viongozi wamekaa tu ofisini,Waziri anarembua tu macho kwa nini wasiige mifano ya viongozi wengine duniani ambao hulazimika kujiuzulu inapotokea raia ameuawa na polisi? Wao wapo tu kimya ofisini ushahidi tumeona vyuo vya mjini Dodoma wameandamana kwa vitendo wanavyofanyiwa lakini Polisi wako kimya wao wakidai haki zao wanakuja na magari ya maji washa kuwamwagia wanafunzi wakati wamepeleka taarifa wanabakwa hakuna majibu tutafika kweli? Au ndio kuongeza uhasama kati ya Polisi na Raia na viongozi wako tu Ofisini hawana wanalofanya kwanini wako maofisini na wanafanya nini