Waziri wa Fedha wa Russia apinga mpango wa Putin ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri wa Fedha wa Russia apinga mpango wa Putin !

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yericko Nyerere, Sep 25, 2011.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  Sep 25, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Waziri wa Fedha wa Russia leo ameupinga mpango wa Waziri Mkuu Vladimir Putin wa kumfanya Rais Dmitry Medvedev kuwa waziri mkuu wake iwapo atarudi tena Kremlin - Ikulu ya Russia,kwa kusema kwamba hatoitumikia serikali mpya.

  Wawekezaji wa kigeni wamekuwa na wasi wasi na dharao hiyo ya Alexei Kudrin baada ya Putin kutangaza kwamba atagombea urais katika uchaguzi wa mwezi Machi mwakani ambao utaufikisha utawaka wake hadi mwka 2024.

  Kudrin ambaye ni mshirika wa Putin amekuwa na tamaa ya kuwa waziri mkuu na amesema amekuwa na tafauti zake na Medvedev ambaye hivi sasa itabidi aonyeshe uwezo wake atakapokuwa waziri mkuu baada ya kulazimishwa na Putin kuachana na ndoto yake ya kuwa rais kwa kipindi cha pili.

  Kudrin mwenye umri wa miaka 50 amesema hajioni kuwemo katika serikali mpya, kauli yake hiyo ameitowa mjini Washington Marekani ambapo amekuwa akikutana na watengeza sera wa kimataifa.***
   
Loading...