Serikali yakiri misaada imepungua.
=======
Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Phillip Mpango amesema nchi inapita kwenye kipindi kigumu kidogo kutokana na wafadhili kupungua kutoa misaada.
Kufuatia hali hiyo, amewataka wanaokusanya mapato kuhakikisha wanasimamia kwa nguvu zote ukusanyaji mapato.
Dk.Mpango ametoa kauli hiyo leo katika Mkutano kati ya Wizara hiyo na Watoa huduma za Serikali katika kukusanya mapato uliofanyika Jijini hapa.
Amesema nchi inapitia katika kipindi kigumu kutokana na wafadhili kupunguza kutoa misaada na wanaotoa misaada pia imekuwa na masharti mengi ya hovyo.
Ameelezwa miongoni mwa masharti hayo ambayo wafadhili wamekuwa wakiyatamka bila aibu kuwa ni wanaopokea misaada hiyo wakubali tabia ya ushoga kitu ambacho nchi haiwezi kukubaliana na masharti hayo.
MY TAKE:
1. Kwanini serikali inataja sharti moja tu la ushoga na kuacha masharti mengine yenye tija kama utawala bora, kufifia kwa demokrasia nchini, wanafunzi wanaopata mimba, sheria ya takwimu, kuzuia mikutano ya vyama vya siasa na ukiukwaji wa haki za binadamu?
2. Kama misaada imepungua kwanini tunalazimisha kuendesha miradi mingi mikubwa kwa wakati mmoja.
CHANZO: Mpango: "Nchi inapita kwenye kipindi kigumu"