Waziri wa Fedha afichua siri ya watu ‘kuchacha’

Waziri wa Fedha afichua siri ya watu ‘kuchacha’

Hata wakijaa bunge zima wachumi hakuna lolote kama bunge litashindwa kukaa kando na serikali na kutenda kazi yake ya kuisimamia serikali kwa kigezo cha chama tawala ni bure tu kama viongozi Wa bunge wataegemea kwenye chama zaidi kuliko kusimamia rasilimali na kufuatwa kwa utaratibu Wa sheria za nchi
Umeenda mbali sana nikama unamsifia waziri kwa ulembukeni na ushamba wake .anaweza kutuonyesha nchi moja wapo ya mfano iliyoendelea kwakuwa na wabunge wengi wachumi !!???
 
Sikio la kufa halisikii dawa,mbona hamjifunzi? au mmeishasahau ubishi wa Mwl.Nyerere na IMF kilitokea nini?

Maadamu Tanzania inategemea wafadhili tukileta ngebe watauwa kabisa uchumi wetu ambao nao unasua sua.

Hivi visingizio vya kushindwa "to read between the lines"mnataka kumbebesha nani mzigo?Punguza jaziba,wazungu wanataka utawala bora na haki za msingi za binadamu,wala sio mambo mengi.
 
Wafadhili hawajachoka,bali wamekata misaada baada ya kuona kanuni za utawala bora zinavunjwa waziwazi bila kutambua haki ya mtu mwingine

Naam, ww umezungumza ukweli japo wanadhani hatuna akili wala hatuelewi lolote. Hata hiyo kujifanya wanawaita wasomi ni baada ya kuona mambo yanazidi kuharibika, sasa wanatafuta mahali pa kufuchia aibu zao ili waseme wameshirikisha wananchi. Zile lugha za kejeli kwamba taifa hili ni tajiri sana na halihitaji misaada sasa imegeuka ni shubiri.
 
Mh. Waziri Mpango amesema kufufua Jumuiya ya Wachumi Tanzania itasaidia kuleta mawazo mbadala yanayotekelezeka

Aidha Waziri Mpango amekiri kuwa Hali za wananchi zimedorora, hakuna pesa mfukoni kwa Sababu Kilimo kimedumaa...

Sasa Serikali imechukua hatua gani kuhamasisha Kilimo na Kuboresha Kilimo? Bla bla bla

Kilimo ndio kinaleta kipato kwa watu wengi, Kwa nini Serikali imeachia kilimo kife?

Kwa nini serikali isiwekeze kwenye Kilimo badala ya Bombadier?

Source: Waziri wa Fedha afichua siri ya watu ‘kuchacha’

Paragraph ya Kwanza tu Waziri amekiri Watu hawana pesa...kwa sababu Kilimo kinadumaa
 
Naam, ww umezungumza ukweli japo wanadhani hatuna akili wala hatuelewi lolote. Hata hiyo kujifanya wanawaita wasomi ni baada ya kuona mambo yanazidi kuharibika, sasa wanatafuta mahali pa kufuchia aibu zao ili waseme wameshirikisha wananchi. Zile lugha za kejeli kwamba taifa hili ni tajiri sana na halihitaji misaada sasa imegeuka ni shubiri.

Tutajenga RELI kwa Fedha zetu wenyewe ---WAMEENDA kukopa

Barabara 6 Ubungo hadi Chalinze -----WORLD BANK wamekataa kutoa pesa

Wameua uchumi, hata makusanyo hakuna....TRA wana haha kupora watu pesa kwa Vitisho

Biashara ndogo za Mama Ntilie wanavamiwa na TRA

Makinikia imepotea hewani
 
Sikio la kufa halisikii dawa,mbona hamjifunzi? au mmeishasahau ubishi wa Mwl.Nyerere na IMF kilitokea nini?

Maadamu Tanzania inategemea wafadhili tukileta ngebe watauwa kabisa uchumi wetu ambao nao unasua sua.

Hivi visingizio vya kushindwa "to read between the line"mnataka kumbebesha nani mzigo?Punguza jaziba,wazungu wanataka utawala bora na haki za msingi za binadamu,wala sio mambo mengi.

Huyu Upare ataleta maafa na MACCM maoga yameufyata Mkia kama mbwe koko
 
Msukuma na lusinde wachumi wabobezi
Wala si hao tu kaka wasiokuwa na maarifa ya chochote, wapo wengi wasiozidi form four. Mbunge wa Nkasi, Korogwe, Magu, Bunda vijijni, Mbeya mjini, Ubungo, Hai, nakadhalika nakadhalika. Bunge lenye composition ya watu wa aina hii haliipi serikali challenge yoyote ya maana. Na wakati mwingine hata kuburuzwa kwao inaweza kuwa ni kwa sababu hii.
 
Maneno ya Waziri ni ya kipuuzi. Atuambie ni wachumi wangapi angalao wana uchumi mzuri wa familia zao ukilinganisha wasio wachumi. Nadhani hajitambui. Afuatilie kumbukumbu za Dunia, atuambie ni nchi gani imeendelea kwa sababu ya kuwa wachumi wengi Bungeni. Atuambie na wale matajiri kumi Tanzania, wachumi ni wangapi?

Kuna wachumi ambao ni wachumi halisi lakini hawana makaratasi. Kuna wachumi wasio wachumi lakini wanaitwa wachumi kwa sababu ya miaka mingi ya kukaa darasani.
 

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema licha ya nchi kuwa na kasi kubwa ya ukuaji wa Pato la Taifa, umekuwa hauonekani katika maisha ya watu walio wengi kutokana na kasi ndogo ya ukuaji wa sekta ya kilimo iliyo chini ya wastani wa asilimia tatu.

Hivyo, amewataka wachumi kuhamasishana kutafuta nafasi za ubunge ili wasaidie wananchi na Taifa wakiwa bungeni.

“Kule tulipo mimi na mheshimiwa Mwigulu, ikitokea Mwiguku katoka wachumi waliopo pale wanahesabika, lakini sehemu kama ile ya kutungia sheria halafu wachumi ni wachache mimi naona ni shida, lakini chombo hiki kinaweza kushawishi kupatikana kwa wachumi wengi ili kunyoosha mambo,” alisema Dk Mpango.

Alisema hayo jana wakati wa uzinduzi wa Jumuiya ya Wachumi Tanzania (EST) katika ukumbi wa Benki Kuu (BoT) jijini Dar es Salaam akiwa mgeni rasmi.

Dk Mpango alisema anaamini kupitia jukwaa hilo wachumi watahamasishana kutafuta nafasi ya kuingia bungeni ili kusimamia mipango ya uchumi ya nchi.

Waziri Mpango alisema changamoto nyingine ya ukuaji wa pato ni ukosefu wa ajira kwa asilimia 10.3 na kiwango cha umaskini kwa asilimia 15, huku ongezeko la watu likiwa asilimia 2.7 kwa mwaka. “Sekta ya fedha imekumbwa na msukosuko wa kuongezeka kwa mikopo chechefu kwa asilimia 12.5 licha ya kiwango cha BoT kuwa ni asilimia tano; riba za kukopa kuwa juu; ongezeko dogo la kiwango cha mikopo na baadhi ya biashara kudorora hasa zile ambazo zilikuwa hazilipi kodi na zenye madeni makubwa,” alisema Dk Mpango.

Nyingine alisema ni wabia wengi wa maendeleo kutoka nje ya nchi kuchoka kutoa misaada ya kibajeti; kuongezeka gharama za mikopo katika benki na taasisi za kifedha za kimataifa na ulaghai unaotekelezwa na kampuni ya uwekezaji kupitia mikataba isiyo na tija kwa Taifa.

Dk mpango alisema ameeleza hayo ili kuwapa wachumi nafasi kupitia EST kufikiri namna watakavyokusanya nguvu na maarifa katika kuongeza kasi ya kuibadilisha Tanzania kuwa kitovu cha uchumi katika bara la Afrika kupitia weledi wao, bidii, uzalendo, uwazi na uwajibikaji.

“Ningependa kuona jumuiya ya wachumi ambayo inajinasibisha kwa umahiri wa kukuza tafiti za kiuchumi, maendeleo ya nchi, mafunzo kwa wachumi kazini, kuratibu jukwaa la mijadala kuhusu sera za kiuchumi, kuibua mawazo mbadala yanayotekelezeka kwa ajili ya kuiinua nchi na kuratibu mifumo ya mahusiano na wachumi wengine,” alisema Dk Mpango.

Awali, Gavana wa BoT, Profesa Florens Luoga alisema hatua ya kurejeshwa kwa jumuiya hiyo ambayo ilikuwa imekufa tangu mwaka 1999 imekuja wakati muafaka kwa kuwa nchi ilikosa jukwaa la kujadili na kuangalia mwelekeo wa uchumi na maendeleo, kutoa tahadhari au ushauri kwa wakati ili kusaidia pale mambo yanapokwenda sivyo.

“Chama cha wachumi ni nyenzo muhimu ya kukuza na kuhakikisha uhai wa wachumi kama ilivyo kwa taaluma nyingine kama vile wanasheria, wahandisi na wahasibu. Chama hiki kinapaswa kuhakikisha uadilifu na elimu endelevu kwa wanachama na hata kuimarisha mafunzo ya uchumi,” alisema Profesa Luoga.

Mwenyekiti wa kamati ya kufufua jumuiya hiyo Geoffrey Mwambe ambaye pia ni mkurugenzi wa Kituo cha Taifa cha Uwekezaji (TIC) aliwaomba wachumi kuiombea jumuiya hiyo iliyosajiliwa kama taasisi isiyo ya kiserikali idumu.

Alisema itakuwa na jukumu kubwa la kusimamia ustawi wa uchumi katika nchi.

“Tutakuwa na jukumu la kuwakilisha maoni ya wachumi, kujadili changamoto za sekta ya uchumi na kuzitafutia ufumbuzi kupitia utafiti, mijadala na uchambuzi wa sera. Tutakaa mbali na sababu zilizosababisha kifo cha jumuiya ile iliyoanzishwa mwaka 1966,” alisema Mwambe.


Chanzo: Mwananchi
Mwigulu kafanya nini kuinua kilimo Iramba?
Sana sana ni kuweka ndani mhadhiri n.a. kutoa mikwara mbuzi kila uchao !

Au ndo maandalizi ya 2020 ili awe mbunge wa jimbo?
 
Waziri asizunguke sana..
Wafadhili WAMEGOMA kutoa misaada kwa sababu ya issue ya UTAWALA BORA, KUMINYWA KWA DEMOKRASIA, UKANDIMIZAJI WA VYOMBO VYA HABARI nk nk, aseme haya.
 
Bunge letu ni bunge huru?kuonyeshwa tu kwa wananchi kwa maana ya Live ni mbinde
 
Dk mpango alisema ameeleza hayo ili kuwapa wachumi nafasi kupitia EST kufikiri namna watakavyokusanya nguvu na maarifa katika kuongeza kasi ya kuibadilisha Tanzania kuwa kitovu cha uchumi katika bara la Afrika kupitia weledi wao, bidii, uzalendo, uwazi na uwajibikaji.

[emoji115] tutalifanyia kazi
Ili kuchangia "maarifa,ujuzi na uzoefu" ni lazima uwe mbunge?
Galileo, Newton,Einstein, Dr.Quashkoor n.k walikuwa wabunge?

Poor reasoning cemented by cramming -( 1+1=2!)
 
Point ya msingi niliyoiona ya mpango ni kuhusu bunge kujaa ma mbumbumbu, ni wakati sasa wasomi tena vijana wanaojielewa (sio mabashite) washike hatamu bungeni, kinyume na hapo hata uwe profesa ukiwa kule bungeni unashuka hadi levo za kina nkamia ili muongee lugha moja.
Mwenye hoja hazuiwi kutoa hoja yenye mantiki na akaeleweka! Tatizo ni saccos ya ccm ambayo elimu ni adui no.1.
Tunaona n.a. kusikia hoja maridhawa za watu kama Zitto ,Lissu, Serukamba,Nape n.a. w engineo zikipingwa/zikipuuzwa n.a. PhD holders kama Mwakyembe,Magufuli,Tulia n.k, kisa "masilahi mapana ya chama!"
 
kati ya mawaziri bomu wa wizara ya fedha huyu pia ni mmojawapo badala ya kuwaambia wachumi watumie taaluma yao kusaidia kuinua uchumi wa nchi yeye anawashauri wakagombee ubunge kama hivyo mbona yeye hajawahi kugombea mpaka ameteuliwa na Rais
 
Wazo zuri la kurudisha jumuiya ya wachumi ila wawe wanashauri serikali bila ya kupepesa macho.
 
Hoja ya maana ni jinsi gani ya kutumia kwa ufanisi Wachumi waliopo Tanzania haswa walio nje ya Bunge kwani hawabanwi na siasa za makundi zisizoleta shibe wala afya!
 
Hivyo, amewataka wachumi kuhamasishana kutafuta nafasi za ubunge ili wasaidie wananchi na Taifa wakiwa bungeni.


Mawazo mgando,

Waende bungeni wakapambane na nani, kwanini wasiwezeshwe wawekeze na kutoa ajira badala ya kwenda kupiga domo na kugonga meza,
 
Back
Top Bottom