kichwa2020
New Member
- Feb 21, 2020
- 1
- 3
Kumetokea tatizo kubwa kwa wamiliki wa shule binafsi Jijini Dar es Salaam mfano Royal Elite Primary School, Anazak Primary School etc kulazimisha watoto wa shule za msingi darasa la mitihani namaanisha darasa la nne na darasa la saba kukaa boarding bila ya ridhaa ya wazazi. Inakuwa ni bila ya ridhaa ya wazazi kwa sababu mazingira unayowekewa na mwenye shule unajikuta huna uwezo wa kukataa hata kama hautaki mtoto wako akae boarding.
Kwanza mwaka wa mtihani hauwezi kumuhamisha mtoto maana anakuwa ameisha sajiliwa na hii taarifa ya kukaa boarding unapewa akiingia tu darasa hilo la mtihani. Pili muda ambao wanataka umlete mtoto shule na muda wa kumchukua unakuwa ni mgumu kuweza kufanya hivyo.
Wanataka watoto wa darasa la mtihani kuanza masomo saa kumi na mbili asubuhi mpaka saa kumi na mbili jioni. Hivyo umlete mtoto shuleni kabla ya saa kumi na mbili asubuhi na umfuate shuleni baada ya saa kumi na mbili jioni. Hii haiko sawa kabisa kwa sababu mwanzo unampeleka mtoto kwenye shule hii hapakuwepo makubaliano ya kwamba mtoto atakaa boarding darasa la nne au la saba.
Shule hizi zinafanya hivi kwa manufaa yao binafsi na huku zikimuumiza mtoto. Kwanza wanawakalilisha watoto masomo ili waweze kupata A nyingi ambazo zitaonyesha shule ina ufaulu wa juu na hii inawasaidia wenye shule kupata wanafunzi wengi na fedha zaidi.
Vile vile kuwaweka boarding watoto, shule inapata fedha zaidi maana mzazi unalipia hiyo huduma ya boarding. Hii haiku sawa maana mtoto wa darasa la nne kuwa darasani masaa 12 sio vizuri kwa afya yake na uwezo wake wa kujifunza ni mdogo sana kwa umri huo.
Wazazi hatutaki hizo A za kuumiza akili ya mtoto. Mtoto wa miaka 8 na 9 ana muda wake kiafya wa kupumzika na madhala yake tunaweza tusiyaone sasa lakini baadae ni makubwa sana.
Kuna wazazi wanaotaka watoto wao wakae boarding ni sawa lakini kuna wengine hatutaki lakini unalazimishwa na masharti tunayowekewa na mwenye shule. Ingekuwa vizuri kama shule imesajiliwa kama boarding na mzazi tangu mwanzo anajua hilo na anakubaliana nalo ila hali haiko hivyo. Vilevile unakuta shule in matron mmoja wakuangalia watoto zaidi ya mia (100) ambao miaka yao ni kati ya 8 na 9.
Wengine hata namna ya kuangalia usafi wao bado. Matron mwenyewe hana mafunzo yoyote ya kuangalia watoto unakuta ni ndugu wa mwenye shule amepewa tu kazi ya umatron. Hakuna nurse wa kuangalia hawa watoto, mtoto akiumwa matron amepewa maelekezo ampe tu Panadol au akikohoa apewe kofta. Watoto hawa ni wadogo kwa umri haifai tuwatesa kwa ajili ya manufaa ya wenye shule.
Mwenye shule anacho angalia ni kupata pesa na kupata wanafunzi wengi tu. Waziri tusaidie utoe mwongozo kwenye hili. Muda wa kuanza masomo shule za msingi uwe unajulikana ni saa ngapi na unaisha saa ngapi ili kuondoa watu wenye tamaa kutuumizia watoto.