Waziri wa Elimu shughulikia suala hili

Mshikawezi Mwizi

JF-Expert Member
Jul 24, 2013
751
375
Ndugu waziri wa elimu, sisi wakazi wa manispaa ya Morogoro tunapenda kuwathirisha matatizo yetu kwako kupitia njia hii ya mtandao pendwa kwani tumejitahidi kutumia njia zingine kwa kuwashirikisha watendaji walio chini yako lakini hadi sasa hakuna kilichotatuliwa.
Ndugu, waziri ikumbukwe mwaka 1966 wananchi tulitoa michango yetu ikiwemo maeneo na nguvu kazi pale ilipohitajika ili tu tufanikishe ujenzi wa shule tulioaminishwa kwamba itawafaidisha wananchi wote bila kujali dini, rangi wala kabila. Hii wala si shule nyingine ni FOREST HILL SECONDARY SCHOOL. Yote haya tuliyafanya tukiitwa Morogoro Society. Ni kweli shule ilijengwa na tukaona matunda yake kwani watoto wetu walipata elimu nzuri bila kujali rangi zao, kabila zao na hata dini zao. Leo hii mheshimmiwa waziri tunaaminishwa kwamba shule hii imeuzwa kwa ISLAMIC FOUNDATION, Shule imefanywa ya kidini, watoto wetu hawana tena uhuru wa kusoma katika shule hii kama dini zao si za upande huu wa walioinunua. Ndugu waziri kinachotushangaza hatujawahi kuona tangazo lolote juu uuzaji wa shule hii. Kingine kinachotushangaza ni kwa nini imeuzwa bila kutushirikisha sisi wadau tuliochangia nguvu kazi na eneo enzi za ujenzi wa shule hii? Kwanini tulilaghaiwa kwamba shule hii itatoa elimu kwa wote bila kujali dini, rangi wala kabila. Ombi kubwa kwako ndugu waziri ni kututhibitishia uhalali wa uuzwaji wa shule hii na kugeuzwa kuwa ya kidini kinyume na makubaliano yetu ili tuweze kudai haki zetu.
 
Back
Top Bottom