Waziri wa awamu ya tatu, Profesa Simon Mbilinyi ainanga Serikali ya Kikwete

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,911
2,891
Waziri wa fedha wa zamani mheshimiwa Simon Mbilinyi ameunanga utawala wa awamu ya nne na kusema ziara nyingi zilizofanywa nje ya nchi kipindi chote cha awamu ya nne zilikuwa hazifanyiwi tathmini ya kutosha na hivyo nyingi zilitumiwa na viongozi kama kufanya utalii na hazikuwa na tija yoyote kwa taifa.

1965641_20190115_100425-1.jpg
 
Aliyekuwa waziri wa fedha wakati wa Serikali ya mkapa mh. Mbilinyi amesema safari za JK nje ya nchi nyingine hazikuwa na tija kwa taifa Bali zilikuwa za utalii na zimeongeza deni la taifa.

Chanzo: Magazeti ya leo
 
Huo ndiyo ukweli wenyewe. Kwa hilo, hatuwezi kuwa Mbuni kuficha kichwa mchangani wakati kiwiliwili chote kipo nje. Safari za JK nje ya nchi ilikuwa ni utalii usiokuwa na tija kwa taifa.
 
Tunamwomba mhusika ajitokeze na kukanusha haya yanayosemwa kwenye magazeti na vyombo vya habari.
 
Tuamini hao kina Steven Segal ndio walikuwa wana tufadhili? Ah! kesha pita na awamu yake ila Haswa naunga mkono maneno ya profesa huyo mheshimiwa ili kuwa hobby yake haelezeki haambiliki na kuna watu wali kuwa na bado wana mtetea,basi hakuna la kufanya,
 
Muwe mnasemaga haya mambo mapema ili kulisaidia taifa! Wakati mambo yanaharibika mnakuwa kimya! mkiona baadaye wenye guts wanaanza kuchukua hatua ndipo kenge nanyi mnaunga msafara!
 
Muwe mnasemaga haya mambo mapema ili kulisaidia taifa! Wakati mambo yanaharibika mnakuwa kimya! mkiona baadaye wenye guts wanaanza kuchukua hatua ndipo kenge nanyi mnaunga msafara!
Walisema sana hadi bungeni hoja hii ilijadiliwa lakini serikali ilikuwa mbogo kukanusha!!Hivyo tutaendelea kusema ili huu utawala mpya usije ukashawishika kuanza safari za kitalii!!!
 
Back
Top Bottom