Waziri Ummy Mwalimu asema uchunguzi umebaini Asma Juma hakubeba ujauzito wa Mapacha

Alijuaje ya kwamba yu na mapacha?

Waliomweleza hivyo ni kina nani na picha walizopiga za Ultra sound huyo bi mkubwa yungali nazo?
 
kawalinda hao madaktari, manake vibarua vilikuwa vinaota mbawa, kawalinda kwa kweli, lakini kweli duniani hakuna haki, haki ipo mbinguni, hapo washaingiza siasa, aisee, hivi huyu mama ana watoto
 
Alijuaje ya kwamba yu na mapacha?

Waliomweleza hivyo ni kina nani na picha walizopiga za Ultra sound huyo bi mkubwa yungali nazo?
Alipiga ultra sound ikaonyesha ana mapacha
Hzo picha inasemekana zimepotea(hospitali)
 
kawalinda hao madaktari, manake vibarua vilikuwa vinaota mbawa, kawalinda kwa kweli, lakini kweli duniani hakuna haki, haki ipo mbinguni, hapo washaingiza siasa, aisee, hivi huyu mama ana watoto
Mkuu usiseme bila ushahidi, wewe ni mzazi? nikiwa na maana una watoto? mimi bado kidogo niwe muhanga wa hizi ultrasound za uchochoroni, nilimpeleka wife enzi hizo ultrasound. Yule sonographa alikua busy na ishu zake huku anamuhudumia wife, mara akaropoka dah mtoto hana mkono aah nimekosea, yani anaropoka kirahisi rahisi huku yuko na ishu zake, akaona makalio ya mtoto akaropoka tena mapacha hawa damn. Nikammind sana yule sonographa kwa kukosa umakini, wakati natoka nikaenda kwa meneja wa hiyo dispensary. Nikamshauri wife tujibane tu twende hospitali ya ukweli sio ultrasound screen haieleweki. Tuna mtoto mwenye afya tu na wala sio mapacha.
 
Alipiga ultra sound ikaonyesha ana mapacha
Hzo picha inasemekana zimepotea(hospitali)

Hii yakupoteza document ipo sana kwenye taasisi za serikali. Unaweza tumia gharama kubwa. Unakuja kufuatilia jambo lako wanakwambia document hatuioni kirahisi rahisi tu.

Na mashaka yote yako hapo ingekuwepo iyo picha japo ni ya kichochoroni ingetatua hili tatizo mapema sana
 
ishu kama hii PUBLIC PROTECTOR ,ndiye angeamua ukweli upo wapi,sasa hatujui nani mkweli hapa Waziri au Mzazi
 
Mungu hashindwi jambo ipo siku hao mapacha wakikua watakuja kutana tu maana damu nzito kuliko maji...hapa naikumbuka ile movie ya marehemu Kanumba, "The lost twins. ."
 
Back
Top Bottom