Waziri Simbachawene, Watumishi wako hawajalipwa pensheni kama mlivyoahidi

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,367
3,778
Mhe. Waziri,

Watumishi wako wana miezi 3 hawajalipwa nauli za kwenda majumbani kwao baada ya kustaafu.

Watumishi wako wana miezi 4 toka wastaafu hawajalipwa Pensheni na mliahidi na Jenister Mhagama kuwa mtarahisisha malipo ya pensheni kuchukua muda mchache sana, pamoja na kujaza fomu zote na kuzipeleka Dodoma miezi 3 kabla ya kuanza likizo ya kustaafu bado hadi sasa pensheni hizo hazijalipwa, baada ya kustaafu hata huo mshahara wa kustaafu haujaanza kuingia.

Mhe. Mawaziri wote Jenister Mhagama na Waziri Simbachawene sio haki kabisa. kaeni kwenye viyoyozi na mnywe chai ya maziwa ila mjue kuna watu wenu wa hali ya chini wanataabika mataani.
 
Mawaziri Tanzania hawana wanachojua WIZARANI labda siasa maana kiutendaji hayo majibu ya pnsheni inatakiwa watoe makatibu wakuu. Ndio maana ningependa kwenye katiba mpya nafasi za uwaziri zisiwepo kupunguza matumizi na kuongeza uwajibikaji badala yake makatibu wakuu waachwe wafanye kazi zao kitaalamu
 
Maisha ya mtumishi lazima yathaminiwe baada ya kustaafu na haki zake zote apewe kwa wakati. yanayo fanyika kwa sasa ni manyanyaso dhidi ya haki za watumishi walio itumikia nchi yao kwa haki na weledi.
 
Back
Top Bottom