Jenister Mhagama, Simbachawene, IGP Simon Sirro tusaidieni tulipwe mafao na PSSSF

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,367
3,778
Mhe Jenister Mhagama, Mhe Simba Chawene Waziri wa mambo ya ndani, IGP Simon Sirro tusaidieni tulipwe mafao yetu na PSSSF, Tumestaafu Mwaka jana mwezi wa 12 Hadi sasa Hatuja pata mafao yetu wala Pesheni hatulipwi. Jana tarehe 1/11/2021 saa 1 usiku tumeenda kukagua akaunti zetu ATM tukiwa wastaafu 4 hamna kitu.

Msemaji wa Serikali anacho kizungumzia kuhusu malipo yetu si kweli, Mara aseme tumekosea taarifa tunahitaji kurekebisha, mara anasema huenda tumetapeliwa sasa tunashindwa kuzieleza familia zetu ukweli. Hii haiwezi kuwa kauli za Msemaji wa Serikali kwa niaba ya Serikali vema akafuta kauli kama hizi, hata tukitapeliwa yeye Msemaji inamhusu nini. Kama Serikali ikiwa haijapata pesa za kutulipa Wastaafu aseme tu ukweli.

Tumeenda mara kadhaa ofisi za Mkoa za PSSSF hawana majibu, wanasema tu zilipokelewa mwezi wa 1 ziko mikononi mwao pale makao Makuu ya PSSSF basi hakuna jibu lingine.

Mhe Jenister Mhagama, Mhe Simba Chawene, IGP Simon Sirro tusaidieni tulipwe mafao yetu PSSSF tusaidieni, mpo ofisini maisha yenu ni mazuri, Nauli zetu pia ambazo zipo kisheria toka tumejaza miezi 2 kabla ya kustaafu hatuja lipwa na madeni mengine ya kwenda wkenye vyeo kama nauli hazijalipwa.

Ombi hili liwafikie popote mlipo au anayesoma awafikishie.
 
SIMBACHAWENA NA IGP wanaingiaje kwenye mafao yenu nyie ni POLISI?

Kwani mmeanza lini kukatwa kuchangia mifuko ya hifadhi ya Jamii?

Nyie (KAMA NI POLISI) si mnalipwa na HAZINA na siyi PSSSF?
 
Nadhani hujaelewa mfumo acha tu, hao unao wazungumzia ni Wajeda ndio wapo huko. Magufuli kabla ya kifo chake mwezi wa 2 akiwa Arusha baada ya kupokea malalamiko alimuelekeza Waziri wa mambo ya ndani NA IGP sirro wawe wanapeleka majina ya wastaafu wao walipwe kwa wakati ikibidi Wiki 2 baada ya tu ya kustaafu, Rais Samia Suluh mwezi wa 4 mwaka huu alisema wataanza kuwalipa wastaafu mafao yao kila mwezi. Basi niishie hapo nadhan umeelewa sasa.
 
Nimekuelewa ila si mnalipwa na HAZINA na si PSSSF?
 
Serikali janja janja! Uswahili mwingi. Walipe hela za wastaafu. Dhuluma haikubaliki hata kidogo.
Pesa za mafao sio pesa za serikali ni pesa za wanachama walikatwa kwenye mishahara. sioni mantiki ya kuona fedha hizi sio muhimu kutowapa wenye nazo. halafu utasikia wanagawa ma bilioni unajiuliza ni ma bilioni upepo kuwahadaa wananchi au
 
Mhe Jenister Mhagama, Mhe Simba Chawene Waziri wa mambo ya ndani, IGP Simon Sirro tusaidieni tulipwe mafao yetu na PSSSF, Tumestaafu Mwaka jana mwezi wa 12 Hadi sasa Hatuja pata mafao yetu wala Pesheni hatulipwi. Jana tarehe 1/11/2021 saa 1 usiku tumeenda kukagua akaunti zetu ATM tukiwa wastaafu 4 hamna kitu.

Msemaji wa Serikali anacho kizungumzia kuhusu malipo yetu si kweli, Mara aseme tumekosea taarifa tunahitaji kurekebisha, mara anasema huenda tumetapeliwa sasa tunashindwa kuzieleza familia zetu ukweli. Hii haiwezi kuwa kauli za Msemaji wa Serikali kwa niaba ya Serikali vema akafuta kauli kama hizi, hata tukitapeliwa yeye Msemaji inamhusu nini. Kama Serikali ikiwa haijapata pesa za kutulipa Wastaafu aseme tu ukweli.

Tumeenda mara kadhaa ofisi za Mkoa za PSSSF hawana majibu, wanasema tu zilipokelewa mwezi wa 1 ziko mikononi mwao pale makao Makuu ya PSSSF basi hakuna jibu lingine.

Mhe Jenister Mhagama, Mhe Simba Chawene, IGP Simon Sirro tusaidieni tulipwe mafao yetu PSSSF tusaidieni, mpo ofisini maisha yenu ni mazuri, Nauli zetu pia ambazo zipo kisheria toka tumejaza miezi 2 kabla ya kustaafu hatuja lipwa na madeni mengine ya kwenda wkenye vyeo kama nauli hazijalipwa.

Ombi hili liwafikie popote mlipo au anayesoma awafikishie.
Nyie ndio mnaobadilishabadilisha majina mbona wenzenu wanaljpwa
 
Ndio uchumi wa Kati unaokuwa kwa 7%.
Naona mwezi huu hawalipwi kabisa sababu hata sisi ambao tumestaafu na kustaafu kwenyewe tumestaafu ( just waiting to kick the damn bucket and exit) hatujalipwa hela ya hazina. Pole sana.
 
Nimekuelewa ila si mnalipwa na HAZINA na si PSSSF?
Unajua serikali ilifanya siasa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii. Zamani kulikuwa na mfuko wa hifadhii kwa wafanyakazi wake, ikawa haipeleki hela, ikaona kuficha udhaifu wake, ikaunganisha na kuwa na mfuko mmoja kwa wafanyakazi wa umma. Nafiki Bado udhaifu uko pale pale, inalipa mishahara ila makato haipeleki PSSSF. Sasa mkistaafu malipo yatoke wapi? Wanawabana waajiri binafsi walipe mifuko, wao hawapeleki
 
Acha kabisa mi kila mwezi naangalia kama makato yapelekwa. So far so good
 
Mkuu kwani wewe ulikuwa unafuatilia makato yako yalikuwa yanapelekwa kwenye mfuko?
 
Mtu analipwa pesa yake kila baada ya bunge kuvunjwa lakini anakua mzito kupigania mtanzania mwenzake ambaye amefanya kazi kwa zaidi ya miaka 30.

Watanzania nadhani kukosa huruma,utu na kutowajibika nidhambi ya asili kwetu
 
Back
Top Bottom