Waziri Simbachawene kuwa wa kwanza kukaliwa kooni na bunge na kuachia ngazi.

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,121
Bunge letu karibu linaanza na bila shaka litakua na mambo mengi sana kuyajadili. Kubwa kabisa ni bajeti iliyopita ivyoferi na bajeti mpya
ilivyoongezwa kiwango cha pesa wakati ya kwaza haijafika hata nusu. Lakn kupwaya kwa utendaji wa wazairi simbachawene hakuwezi kuachwa kama alivyo. Kupwaya huko kunatokana na waliochini yake hususani mkuu wa mkoa wa Dar. Tukumbe bunge liliwaita watendaji walio chini yake huku yeye akionekana kutochukua hatua yeyote huko nyuma.

Kabla hata hawajakutana na kamati ya bunge watendaji hao waliochini yake mmoja akitibua tena .
Yaan ingekua shule tungesema kabla adhabu ya kulima kipande chako kama adhabu unakosea tena. Sijui kamati ya shule itakufanya nini. Ni kweli mkuu wa mkoa aliitwa na alijadiliwa . Lakn tukumbuke kamati hufanyia kaz hadidu walizopewa tu!! Hivyo haya madudu ya kuvamia clous na kumchafua mchungaji gwajima hawakupewa wayajadili.hata hii kubwa kabisa , skendo ya kutumia jina la mtu katika masomo yake haijajadiliwa!

Kuna watu wanabeza lakn wanashindwa kutoa majibu kwa makosa hayo. Hasa lililo wazi la kuvamia clous hadi kupelekea aliyekua waziri wa habari kufukuzwa. Haiwez kuwa ishu ya kitoto kama imeondoka na waziri. Ni ama waziri aliye pita alikua sawa ama mamlaka zilizomtoa zilikosea kwa kumwacha mkosaji na kumwondoa msafisha uchafu.
Na mtu pekee atakaye lemewa kabla ya kufika kwa waziri mkuu ni waziri wa tamisemi mheshiwa simbachawene. Hajasema chochote tangu sakata hili lijitokeze. Zaid zaid alionekana anapiga makofi pale rais alipomtetea mkuu wa mkoa kwa kumwambia piga kazi. Kupiga maokofi kwake na vicheko vinaashiria anaunga mkono uvamizi ule. Tizama mwenyewe kwenye video hii hapa.




Binafsi naona Simbachawene kakalia kuti kavu, sijui mtizamo wa wenzangu. Kuna wengine wasimamia kwenye msimamo wa rais kumkingia kifua mkuu wa mkoa lakn tukumbuke bunge halifanyii kazi kauli za rais watataka kujua wizara inasemaje juu madudu hayo. Na yeye ndio boss wa wakuu wa mikoa. Tusubiri tuone.
 
Wewe umewahi kuachia ngazi wapi ama unafikiri ni suala jepesi kiasi hicho
 
Tatizo la msingi hapa ni kuwa Mawaziri hawafanyi kazi zao kwa utashi wao, ni mpaka wapokee miongozo kutoka Ikulu jambo ambalo linawadumaza weledi wao katika kutimiza majukumu, kiukweli Uncle Magu anawanyima uhuru ni kama Vikaragosi tu vya Mchawi Karaba kwenye sinema ya Watoto Kirikou.
 
Tatizo la msingi hapa ni kuwa Mawaziri hawafanyi kazi zao kwa utashi wao, ni mpaka wapokee miongozo kutoka Ikulu jambo ambalo linawadumaza weledi wao katika kutimiza majukumu, kiukweli Uncle Magu anawanyima uhuru ni kama Vikaragosi tu vya Mchawi Karaba kwenye sinema ya Watoto Kirikou.
hili jambo limejadiliwa mno kwenye mitandoa ya kijamii n.k bila hatua yoyote kuchukuliwa na wahusika hadi sasa inatia kinyaa kulisikiliza maana kila kitu ki wazi.acha hoa wabunge sasa tuwaone kama ni wawakilishi wetu kweli au nao ni wasaka tonge t u.kama kawaida yao watafunika kombe mwanaharamu apite kama bahasha zitatembea.kwani mangapi tulitegemea watukomboe lkn ikawa surprise kwetu?sana sana wapinzani watajitahidi ingawa hawaatafua dafu kwenye kwenye swala la NDIOOOOO!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Walipigwa mkwara mzito kwa hiyo wabunge wa ccm hawawezi kufanya jambo lolote la maana
 
Watu mnapenda kupiga porojo sana. Nilikuwa najiuliza Mnyama Chawene kafanya nini tena, kumbe porojo zile zile za Wauza mihadarati
 
Waliojifanyia kazi utawala wa kikwete bila ya kuingiliwa, nini tija Yao?
Au kichwa chako hakitunzi kumbukumbu?
 
Back
Top Bottom