Waziri Simbachawene awashukia Lowassa na Dr. Magufuli

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,517
Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene amewataka wanasiasa kutotumia mgawo wa umeme kama turufu ya kisiasa.

Waziri Simbachawene amesema umeme ni jambo la kitaalamu na si la kisiasa. Amesema uzalishaji na usambazaji wa umeme ni suala la kitaalamu.

Simbachawene ni kama amewajibu wagombea wa Urais Edward Lowassa na Dr. Magufuli, ni wagombea hao waliozungumzia mgawo wa umeme kwenye mikutano yao ya kampeni. Wote wawili waliwapiga mkwara Maafisa wa TANESCO kwa kukatakata umeme.
 
Simbachawene kaingizwa mkenge. Mbona toka vitisho vitolewe hali ya umeme imekuwa nzuri. Kwangu toka umeme toka juzi unawaka bila matatizo
 
Nimesharekebisha. Amewataka kutotumia.. haya karibu kwa mjadala
Mkuu, hakuna mjadala wowote hapa. Simbachawene kavurugwa japo anaweza kujitetea kuwa ameongea kitaalam. Tunaojua mchezo uliokuwa unachezwa tunabaki kumcheka tu
 
Wakati huohuo Katibu Mkuu Ombeni Sefue amekiri kuwa Serikali imeshindwa kufikia malengo ya MDGs kwa sababu ya mipango hafifu, likiwemo hili la umeme:


Dar es Salaam: Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema serikali haijaweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa -malengo ya milenia ya mwaka 2000 ambayo kwa sasa yananamaliza muda wake- kwa sababu ya kukosa mipango thabiti ya jinsi ya kuyafanikisha.

Malengo ambayo hayakufanikiwa ni sekta ya elimu,kilimo, afya, ,usawa wa kijinsia,uhai wa viumbe juu ya ardhi,upatikanaji wa maji safi na usafi wa mazingira,upatikanaji wa huduma rahisi ya nishati ,ukosefu wa ajira na ukuzaji wa uchumi.

Ombeni alitoa kauli hiyo leo wakati akifungua mkutano wa wadau wa takwimu ulioandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), uliolenga kuelimishana juu ya kukamilika kwa utekelezaji wa malengo ya milenia(MDGs) na kuanza kwa Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na jinsi ya kushirikiana katika kuhakikisha takwimu za viashiria vya mpango mpya -zinapatikana kwa wakati.

“Kama mnavyofahamu utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia - MDGs ulikuwa ni wa miaka 15 kuanzia mwaka 2000 hadi 2015. Mpango huu -hatukuweza kufanikiwa kutokana na kwamba tuliwekeza zaidi katika kujenga shule nyingi na vituo vya afya vingi,na kuhamasiha zaidi tukasahau kuwa tunatakiwa kupanua wigo wa ajira utakao saidia kukuza uchumi wa mtu mmojamoja,”alisema Sefue.

Sefua aliyataja malengo mengine ambayo hayajafanikiwa kuwa ni kukosekana kwa -viwanda na miundombinu, amani na utawala wa sheria na tofauti ya kipato baina ya nchi na nchi na ndani ya nchi.

Mengine yaliyoshindwa kufikiwa ni kutokuwepo kwa miji na jamii endelevu, kuwajibika katika uzalishaji, kuchukua hatua za haraka kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na madhara yake.

Chanzo: Mwananchi

My take: Kwa siasa hizi za kwetu za ulaghai bado tuna safari ndefu sana kujikwamua.
 
Magufuli mikwara mingi, jengo la Tanesco lilimshinda kuvunja ataweza kuwawajibisha viongozi wake?
 
Akisema hivyo, atambue kila ahadi zinazotolewa zina wataalamu wake. Kila kitu ni cha kitaalamu, chawene afundishwe nini maana ya siasa ndpo ajitetee
 
Ukweli kuna tatizo Tanesco inabidi watuambie tuwaeleweje.

Leo kwetu siku ya tatu UMEME haukatiki !!! how come??!!
 
Lakini kiongozi, kama Mtera haizalishi, (refer ITV news leo usiku) Simbachawene atatoa wapi umeme? Lowassa na Magufuli wamekurupuka.

Kama kweli uzalishaji wa umeme ni suala la kitaalam kama anavyodai, kwa nini alitamba siku chache zilizopita kwamba mgawo wa umeme utakua historia, muda aliowatangazia wananchi umepita na mgao ndio kwanza unaongezeka.

Asiwe mwepesi wa kusahau aliyoyasema kwa wananchi, kama hataki kua mwanasiasa asigombee ubunge!
 
Sijawahi kusikia waziri mjinga kama huyu.hivi anavyosema suala la umeme siyo la kisiasa anataka wananchi waulize kitu gani kwa viongozi wao huku wako gizani? Please please Dr.Magufuli huyu jamaa hafai kuongoza wizara yeyote kwa majibu haya.alitaka suala la umeme tukazungumzie wapi? Pumbavu sana
 
hv aliyesema kukatika umeme itakuwa historia baada ya matumizi ya gesi kuanza ni akina nani,hv simbachawene anajua anachokiongea au ulimi unaendelea kuteleza,yeye akatae asikatae ni waziri mzembe ndio maana wizara imemshinda na umeme hakuna,Magufuli na Lowasa wanasema wazembe kama hao mwisho wao ni kwenye serikali hii ya kizembe ya JK.
 
Lakini kiongozi, kama Mtera haizalishi, (refer ITV news leo usiku) Simbachawene atatoa wapi umeme? Lowassa na Magufuli wamekurupuka.

kazi yake ni kuhakikisha tunapata umeme,kama hawezi arudi kwenye kazi yake ya ukondakta..
 
Back
Top Bottom