Waziri Simbachawene apendekeza Watumishi wa Umma wasiingie ofisini na simu


Naunga mkono hoja,tena washonewe na sare kabisa wavae kama wanafunzi wa shule ya msingi. Pia wanawake wasiruhusiwe kusuka.

Hii itapunguza sana ufisadi na wizi wa mali za umma.
Hili pendekezo linawahusu pia waliopandisha bei ya invoice ?
 
Mhe. Simbachawene ameongeza kuwa, mtumishi anaingia kazini na simu ambayo ina makundi mengi, akianza kuwasiliana na makundi matatu tu saa moja ya kazi imeondoka na kwa kuwa ana makundi ya majirani, vikoba na mengineyo hivyo akiendelea kushiriki kinachojadiliwa unakuta matumizi ya simu yanachukua muda mwingi wa kazi

Utumishi

NDIO MAANA KUNA TOFAUTI YA MTOTO NA MTU MZIMA.....

IKIWA MTU MZIMA ANAPO GEUKA MTOTO LAZIMA TU M TREAT KAMA MTOTO....

MM KAZI NAZO FANYA NINA DEAL NA WATU MUDA MWINGI ILA SIMU HAIJAWAI KUA TATIZO, TATIZO NI WATU WENYEWE TENA WATU WAZIMA WANATAKA WAANZE TRITIWA KAMA WATOTO WA MSINGI AU SECONDARY SCHOOL.....
 
Mawasiliano mfano simu ni sehemu ya kazi kwasasa ndomana walimu wakapewa vishikwambi...
huyu sindio yule mwanae mlevi alisumbua askari eeh? Like father like son!!
Shughulika watumishi wapande madaraja ipasavyo acha kujishughulisha na maujinga.
 
Haya majitu ni majinga sana ,yanaiba huko harafu wanakuja kusumbua Watumishi.
 
Litakuwa linawahusu hao watumishi walioko wizarani maana hawa wengine huku chini sijawahi enda ofisi yoyote nikakosa huduma kisa mtu anabembeleza mchepuko au danga.
Thanks mkuu, maana Kila baya watumishi huwa tunaonekana shida ila Kuna wananchi wasema kweli kama wewe wachache sana. Asante sana mkuu
 
Reactions: K11
Ujinga ndio unaanziaga hapa.Akitaka kwenda kutembea ofisi fulani atawatafuta kwa mguu
 
Utumishi katika nchi ina matatizo mengi na makubwa kuliko hilo dogo analobainisha huyo Chawene .Walimu na manesi aliowatolea mfano ni watumishi wenye matatizo lukuki yakiwemo ya maslahi madogo na kutolipwa malimbikizo ya mishahara yao kwa wengine tangu 2017 hayo magroup wataingia kwa saa nzima data ataweka yeye
 
Halafu sio vizuri kuwafanya wafumishi wenzio kama sio binadamu wasio na haki,yapo mazuri mengi wanafanya kwa taifa lao licha ya changamoto nyingi walizo nazo.
Tujifunze kuwakosoa kwa hekima na pale inapobidi pia tuwapongeze isionekane wote hawana jema.
Kuna miaka kulikuwa na nidhamu public service kwani husikii wenzio wakisema?Simu hazikuwepo?
Fanya utafiti wako vizuri,njoo na suluhu lenye afya kwa kuzingatia mizania sawa hautapigwa mawe.
Kwa hili umeteleza pakubwa.
 
Mawazo,,fikra,,maono,, ya viongozi wetu wakati mwingine yanashangaza sana,,,kuna mambo mengi sana yakufanyia kazi kwa wafanyakazi wa serikali,,Uache kuzungumzia uboreshaji wa mazingira yao ya kazi,maslahi kwa wafanyakazi,,,promesheni za motisha kwa wafanyakazi ili kuongeza chachu katika utendaji,,,kubuni na kuunda mifumo bora ambayo itakuwa bora na italeta angalua ahueni kwa hao wafanyakazi nk,,,,Simu kweli ndio inakuwa ajenda ya maana na kuzungumzwa??Na makamera juu kwa ishu ambayo haina maana kabisa,,,na wala sidhani kama ni tija kwa sasa kwa hao wafanyakazi,,,,Ajenda nzuri,,kanuni na sheria bora wanajitungiaga wao kwa maslahi yao,,,wengine wasiwe na simu kwa ulimwengu huu wa sasa wa teknolojia simu haikwepeki,,popote pale!!!Akajipange aje na hoja za maana!!!
 
Reactions: Cyb
Wow 🤣🤣🤣🤣🤣

Kweli tumebalikiwa na ujinga tele. I mean what the fuc*k is wrong with viongozi hawa??

Keep recycling and reusing the same people and hoping for a different outcome!

WOW!
 
Ningemuona ana akili kama angekuja na mpango wa kuhakikisha kila mtumishi wa umma madai yake yaliyohakikiwa yanalipwa ndani ya miezi miwili na yale yaliyobado kuhakikishiwa yanalipwa ndani ya miezi minne ili hao watumishi wasifanye kazi kwa kinyongo na kuongeza ufanisi wa kuwahudumia watanzania.Tutamuona huyo jamaa atakavyoperform naona anajaribu kudeal na vitu minor sana hakuna Mtumishi atajizuia kutumia simu kwa masaa 8 simply ameagiza huyo Simbachawene
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…