Waziri Ndejembi atatua Mgogoro wa Ardhi Njombe, Wananchi na KKKT

Waziri Ndejembi atatua Mgogoro wa Ardhi Njombe, Wananchi na KKKT

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi leo Aprili 3, 2025, amefanya ziara ya siku moja mkoani Njombe kwa lengo la kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa muda mrefu wa ardhi kati ya wananchi wa eneo la Lunyanywi na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Njombe (KKKT).

Katika ziara hiyo, Mhe Ndejembi alisikiliza pande zote wakiwemo viongozi wa kanisa wakiongozwa na Askofu wa Dayosisi ya Njombe, Dkt. George Fihavango, Viongozi wa Mkoa na Wilaya, Kata na Kijiji.

Baada ya kupitia nyaraka za umiliki wa ardhi na kujiridhisha na uhalali wa eneo husika, Mhe. Ndejembi amewataka wananchi wote waliovamia eneo la Kanisa kuacha mara moja na kusubiri maamuzi rasmi ya Serikali.

 
Back
Top Bottom