Waziri Nchimbi afukuzwa kwenye mazishi ya mchungaji wa aliyeuliwa kwenye vurugu za kidini

Status
Not open for further replies.
Acheni mambo ya ajabu, mmeshindwa hata kumkoa, au kumpiga kibao aaa.......? Ina maana amakuja kwa miguu? Kwa nini msingelitia shangingi lake kiberiti? Yaani mnesikitisha sana kwa kumuacha huyo Mbulula aondoke salama.
ofuuuu Master Peace huyooo, je akija ant peace itakuaje?
 
Leo mida ya saa tano za asubuhi waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi (MB) amefuzwa na wananchi waliokuwa wamekusanyika nyumbani kwa marehemu kuaga mwili wake. DK. NCHIMBI alifika na Story za kuomba suluhu kati ya waislam na wakristo.

Alipofika tu akaanza kusema ameleta rambirambi ya serikali but wananchi wakasema aondoke hana hoja maana serikali ndiyo chanzo cha vurugu kwa kuwakumbatia waislamu. Hii yote ni mwendelezo wa waziri NCHIMBI kushindwa kutatua mgogoro huo hapa Geita. Habari zilizopo ni kuwa makanisa yote yameungana, msiba huu umekuwa wa kihistoria mkoani GEITA kwa kuvuta hisia za watu wengi mkoani hapa

Labda Macho yangu yana pazia, Hii taarifa imepostiwa lini na sasa hivi ni saa ngapi?
 
Namkumbuka sana alivyohusishwa na kifo cha Amina Chifupa (Japo sijui kama ni kweli). Lakini anavyoonekana sasa na kuvaa miwani ya black ni ishara mbaya sana kwa uhai wa nchi
 
I am christian, naielewa hoja ya christian nao kuchinja. Kwa ajili ya undugu na hawa wenzetu suluhisho ni sisi christian kuiacha agenda hii. Tunaweza kusema kuwa na bucha ya christian everywhere but this will separate us. Vita vyetu sio vya nyama na mwili.

Acha unafiki kaka, siku zote hayakuwepo haya mambo ya nani inabidi achinje. Suala la waislamu kuchinja limepewa na nguvu na serikali na kuwa-supported na chama chako, na hiyo ndio sababu kubwa ya mtafaruku uliopo sasa hivi. Bila viongozi wenzako kutoa matamko ya kuhalalisha waislamu kuchinja, leo tusingekua tunaongelea suala la vifo. Hivi mlijiuliza kuhusu KITIMOTO atachinja nani wakati wachinjaji hawataki hata kumuona? Kama hakuna mchinjaji, si mnaamaanisha KITIMOTO haruhusiwi nchi hii? Kwa tafsiri ya haraka, ni kama mnataka kuifanya Tanzania nchi ya kiislamu wakati katika ya nchi yetu inasema nchi yetu haina dini. Kishauri chama chako kitumie akili katika maamuzi hasa yale yanayoweza kupoteza umoja na mshikamano wetu ulioasisiwa na baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere.
 
I am christian, naielewa hoja ya christian nao kuchinja. Kwa ajili ya undugu na hawa wenzetu suluhisho ni sisi christian kuiacha agenda hii. Tunaweza kusema kuwa na bucha ya christian everywhere but this will separate us. Vita vyetu sio vya nyama na mwili.

tatizo sio kuchinja.... Tatizo ni wengine kuwa special sana kutaka kuingilia mpaka mamlaka ya wenzio. Kwa nini walienda kufanya vurugu kwa kuwa ng'ombe alichinjwa na wakristu? hilo ndo chanzo na haswa pale serikali inapofumbia macho kwa makusudi uozo huu au inafumbia macho kwa malengo maalum ya divide and rule.....? maana mnatuchanganya wananchi

Kulikuwa na sababu gani za kutoa matamko yasiyo na kichwa wala miguu? Kulikuwa kuna ugumu gani wa kusema kila mmoja atachinja kitoweo chake kwa imani yake? Very simple na tatizo limekwisha mambo yangerudi normal? Mana msibani si lazima ule pilau au unywe uji kama imani haikuruhusu...kuhudhuria tu kunatosha.

Viongozi wa serikali watumie busara hata za kuazima inapokuja maswala sensitive kama ya dini. Ni rahisi utu kupotea pale jamno lolote linapohusu dini. Unless nia ni kugawa wananchi?

Kuchinja kusingeleta vurugu kama busara ingetumika toka mwanzo. Mara ngapi kuna mihadhara ua kukashifu ukristu kuna hatua zilizochukuliwa? Waliichoma moto makanisa mbagala hatua gani zimechukuliwa? Mara ngapi kwenye hata mitandao ya kijamii kuna kurushiana kashfa za dini? as if tanzania kuna dini mbili tu?

Serikali inapaswa ichukue hatua za makusudi kuzuia hilo. Isichanganye dini na siasa. Ni bomu ambalo halitoweza kuteguliwa.

I am christian, naielewa hoja ya christian nao kuchinja. Kwa ajili ya undugu na hawa wenzetu suluhisho ni sisi christian kuiacha agenda hii. Tunaweza kusema kuwa na bucha ya christian everywhere but this will separate us. Vita vyetu sio vya nyama na mwili.
Baada ya kuona Dr. Slaa kawashika vibaya kwenye uchaguzi mkuu 2010 mkaamua kuingiza masuala ya udini. Mliona "liwalo na liwe" ili mradi mpate madaraka. Matokeo yake ndio haya sasa.

Sasa hivi mumeanzisha lingine la "Ukanda". Madhara yake yatakuwa makubwa kuliko.

Ukichanganya huo udini na ukanda mnaoueneza, nchi yetu mnaipeleka kubaya sana.
 
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba acheni unafiki udini,ukabila na ukanda mmeuasisi wenyewe sasa mnavuna matunda yake.

I am christian, naielewa hoja ya christian nao kuchinja. Kwa ajili ya undugu na hawa wenzetu suluhisho ni sisi christian kuiacha agenda hii. Tunaweza kusema kuwa na bucha ya christian everywhere but this will separate us. Vita vyetu sio vya nyama na mwili.
 
Acheni mambo ya ajabu, mmeshindwa hata kumkoa, au kumpiga kibao aaa.......? Ina maana amakuja kwa miguu? Kwa nini msingelitia shangingi lake kiberiti? Yaani mnesikitisha sana kwa kumuacha huyo Mbulula aondoke salama.
wanazidiwa hata na wamakonde viva wamchinga maana wangeshatia shangingi moto,pambaf
 
Mwigulu Nchemba kama kada wa CCM nakushauri tu nenda kawaambie wenzio walio asisi UDINI warudi kuwaomba radhi watanzania na waanze kuwaadabisha wale wote wanaotumia majukwaa kuwaambia vyama vya upinzani vina udini,ukanda nk.
Pili wale wote wanaotukana dini za wenzano majukwaani,kwenye mitandaoni,redioni na hata kwenye nyumba za ibada na hata kuweka chuki miongoni mwa waumini wa dini tofauti wachuliwe hatua kali na mmojawapo ni UStadhi Ilunga wa Mwanza achukuliwe hatua sasa.
 
Acheni mambo ya ajabu, mmeshindwa hata kumkoa, au kumpiga kibao aaa.......? Ina maana amakuja kwa miguu? Kwa nini msingelitia shangingi lake kiberiti? Yaani mnesikitisha sana kwa kumuacha huyo Mbulula aondoke salama.

Lazima ujue kuwa wakristo sio watu wa fujo isipokuwa wapenda amani na wahubiri upendo tatizo ni pale uzalendo unapowaishia.
 
I am christian, naielewa hoja ya christian nao kuchinja. Kwa ajili ya undugu na hawa wenzetu suluhisho ni sisi christian kuiacha agenda hii. Tunaweza kusema kuwa na bucha ya christian everywhere but this will separate us. Vita vyetu sio vya nyama na mwili.

Mkuu Mwigulu Nchemba, ninamashaka na Ukristo wako, wazo lako ni sawa na mpango Shetani kumshawishi Yesu atende dhambi. Tatizo lako Mwigulu ccm ilishakomba akili zako zote ndo maana upo hapa kutushawishi wakristo tuwe tunakula nyama zilizochinjwa kwa Mungu wa waislamu (Alah).
 
Am Muslim na nawaunga mkono wakriston

1. Je nguruwe tuletewe tuchinje sisi waislam?

2. Kuna madahara gani mtu kujichinji a ngombe
wake na akapitishwa na dr kuwa nyama ni salama na akawauzia wanao itaka na wasio itaka wakanunue kwingine?

3. Umeshawahi kufika machinjioni ukaona weanavyo chinja? Je wajua kuwa hata hivyo wanavyofanya sio uislam na tunalishana vibudu kila siku? Labda ni kudokeze tu, uchinjaji wa kislam unataka mnyama achinjwe akiwa hai na sio akiwa amezima na kinachofanyika sasa ni ngombe anapigwa nondo au anapigwa short ya umeme na kuzimia ndipo anachinjwa, na hii tayari ni Kibudu.

Vyakula mahotelini, mama lishe na kwenye migahawa utajuaje kama mnyama alichinjwa na muislamu? Sioni tunachoshindania, wanyama wanaochinjwa kwa ajili ya biashara tuwaachie nduge zetu waislamu ili nao wao waweze kushiriki hicho kitoeo
 
Nchimbi ni moja kati mawaziri dhaifu sana,uwezo wake ni mdogo sana,ukimtazama hata anavyoongea utaona jinsi uwezo wake wa kufikiri ulivyo mdogo,aidha elimu yake pia ni zile za kununua,kwa hivo msimshangae kwanini ameshindwa kudeliver kwenye wizara hii....tumshangae JK kwa kumpa wizara nyeti mtu dhaifu kama Nchimbi..
 
huyo aliyemteua amepwaya vipi achague watu waliomzidi uwezo?wanatafuta madaraka kwa kutumia mambo ya hatari ambayo hata jamii zao kwayo hazitasalimika mtu yeyote aitumiaye dini kama ngao yake aweza kuangamiza kizazi chake na jamii nzima.ninyi waacheni waendelee na upuuzi wao wafikirie kama wao na watoto,mamawajukuu mama zzao wadogo watabaki salama wakati utatufafanulia yote haya.
 
I am christian, naielewa hoja ya christian nao kuchinja. Kwa ajili ya undugu na hawa wenzetu suluhisho ni sisi christian kuiacha agenda hii. Tunaweza kusema kuwa na bucha ya christian everywhere but this will separate us. Vita vyetu sio vya nyama na mwili.

Mwigilu... Mshaurini raisi Kikwete kulimalizA hili kwa staili ya mzwe Ruksa.... Sisi hapa JF. Hatutaki kujua Kama wewe ni Christian au muislam maana haitusaidii chochote !
 
I am christian, naielewa hoja ya christian nao kuchinja. Kwa ajili ya undugu na hawa wenzetu suluhisho ni sisi christian kuiacha agenda hii. Tunaweza kusema kuwa na bucha ya christian everywhere but this will separate us. Vita vyetu sio vya nyama na mwili.

Shida yako Mwigulu unafikiaga hatua unapenda zaidi chama kuliko hata Mungu/dini yako. Waambie viongozi wenzio, ni kweli kulikua hakuna shida yeyote hapo mwanzao, viongozi wenzio ndio waliochafua hali ya hewa na kuwaambia Wakristo wenzio eti suala la kuchinja ni IBADA kwa Waislam, labda wewe ni mkristo jina, hata Biblia huijui, kunasehemu imeandikwa msile kilichochinjwa kwasadaka ya miungu, kasome wakoritho utaona, zamani hao wakristu wenzio hawakujua kama Waislam wanafanya IBADA kwa kuchinja, sasa wameelewa, kwenye vikao vyenu, waambie hao wenzio, wanapokuja kutatua migogoro wawe wanakuja na busara sio kuja na sifa za majina yao ya utani kama Tyson, hayo ndio matokeo yake, ubabe hua mara zote hausaidii hata kidogo!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom