Hess
JF-Expert Member
- Feb 27, 2012
- 593
- 675
Imenichukua siku kadhaa nikiwaza ni lini Waziri Mwigulu Nchemba na IGP Mangu watajiuzuru au kufutwa kazi. Vifo vya askari wetu kwa kuuliwa na majambazi umekuwa wimbo usiokoma. Yalipotokea mauaji ya askari kule Mbande Mwigulu ulionekana na sare za jeshi watoto wa mjini husema ulikwenda kuuza sura, hakuna mkakati wowote ulioufanya kuhakikisha mauaji ya aina hii kwa walizinzi wetu wa amani yanakoma. Ulikuja na matamko ya kisiasa utadhani unamjibu Mdee bungeni wakati kuna maiti 4 za askari wetu zilikuwa zimelala. Hii ilitosha kwa wewe kuanza kujipima kama unafit kwenye nafasi hiyo.
IGP Mangu nawe umekuwa kama mwanasiasa, umekosa weledi na mbinu kuhakikisha mauaji haya yanakoma. Umekuwa unaimba nyimbo za kina Makonda mithili ya Kasuku. Unataka askari wetu wangapi wafe ndo uchukue hatua? Kuna nini kigumu kuzuia mauaji haya?
Tukio la juzi la askari wanane kuuawa na majambazai (inasemekana jambazi mmoja) huko Mkurunga linatosha kuwafanya mjiuzuru au mfukuzwe kazi. Haiingii akilini askari wanane wanapoteza uhai wakiwa kazini na nyie mko police officers mess na glass mkononi. Tamko la Nsato ni muendelezo wa matamko ya kisiasa yasiyo na suluhu kwa uhai wa askari wetu. Nsato anasema hakuna ugaidi Tanzania na wakti huo huo kuna masheikh wako gerezani bila dhamana kwa kesi za ugaidi... lini mtaacha siasa kwenye uhai wa askari wetu?
Vifo vya askari wa juzi ni muendelezo wa vifo katili vya askari wetu huko Mkurunga. Ni miezi michache tu imepita mkuu wa polisi huko kibiti aliuawa pamoja na askari wengine kwenye kizuizi cha barabarani baada ya majambazi kuteka eneo hilo... Mnataka afe nani ndo mfanye kazi?
Juzi nchi imeingia kwenye taharuki za matukio ya kutisha ya utekaji... Ilianza kwa Ben Saanane, mkakaa kimya sababu ni mpinzani, huyu ni mtanzania, mnalipwa kwa kodi zake ili awe salama. Ikaja kwa Roma na ikahusishwa na Bshite lakini hakuna mmoja wenu aliyepaza sauti hata ya kulaani tu tukio hili. Bunge likapaza sauti hamkujali.
Nilitegemea tukio la Staki Shari lingekuwa tukio la mwisho kwa watanzania kusikia kuhusu vifo vya askari wetu lakini kwa either kukosa umakini wenu au kutokujali au kwa sababu ya uwezo wenu mdogo kwenye idara hii, matukio haya hayajakoma. Ni muda mwafaka sasa mpishe hizo ofisi za umma kuna watanzania wengi wenye uwezo nazo, wapo kina Adadi Rajabu watatusaidia sana kwa nafasi ya Mwigulu.
Mwigulu unaweza kuandika barua sasa kwa Rais na mweleze kiatu alichokupa kinakupwaya sana. IGP Mangu, linda heshima yako kwa kuachia nafasi hii. Waachie wenye weledi watakaoishirikisha jamii kwenye ulinzi. Siku ulipoambiwa askrai waogopwe na raia ilitosha wewe kujiuzuru na sio kutekeleza agizo hili. Raia na askari lazima wafanye kazi pamoja.
[HASHTAG]#nchemba[/HASHTAG] na Mangu mtupishe sasa. Muda mwafaka kabisa