Memento
JF-Expert Member
- Jun 13, 2021
- 4,423
- 9,962
Kulitokea ajali mwanza ya waandishi wa habari na watu wengine, ajali ilibeba simanzi na huzuni nchi nzima.
Waziri mwenye dhamana Nape nae hakua nyuma kushiriki bega kwa bega kuiwakilisha serikali.
Lakini akiwa huko tarehe 12 mwezi huu alitoa siku 7 wale waliokufa ajalini wawe wamelipwa chote wanachodai na kutishia kuwa leseni za hizo media anazo yeye hivyo anawapa siku 7.
Kama kawaida wapo waliopongeza na wapo waliokosoa kuwa kwa utaratibu wa kimahakama na namna ya kupata warithi ni ngumu kukamilika ndani ya siku 7.
Hivyo agizo la waziri Nape lilikua haliko sawa pengine hakujua sheria inavyotaka jinsi ya kuwapata warithi.
Sasa ni siku 14 na bado taratibu hata za kupata warithi hazijakamilika achilia mbali hayo malipo aliyotaka walipwe.
Je, Waziri anasemaje? Alikurupuka au kawaongezea muda.