VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Ndugu Nape Nnauye ni ima hajui yeye ni nani au 'anataka kutenda zaidi'. Ndugu Nape Nnaye ni Waziri mwenye dhamana ya mambo ya Michezo, Habari na Utamaduni. Ni kiongozi wa kiserikali katika ngazi ya Uwaziri. Ni mtu mkubwa nchini. Lakini, ananiangusha.
Leo, hapa Ofisi Ndogo Lumumba, Nape ameshiriki kumpokea na kumpongeza mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Ally Samatta. Samatta amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa soka baraniAfrika kwa wachezaji wanaocheza soka lao barani humu. Pongezi hizo ziliongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Dr. Jakaya Kikwete.
Ilikuwa ni hafla ya kichama. Yeye hakupaswa kuwa mbele kwenye hafla ya leo. Kwa kujiweka mbele, amechanganya mambo ya kiserikali na kichama. Ima ameshau kuwa yeye si tena 'kiongozi wa kichama' au ametaka kujionesha kuwa anawajibika kichama na kiserikali. Lakini, anapaswa hima kujitenga na chama. Asichanganye mambo.
Kama Mbwana amealikwa na kukubali mwaliko wa CCM, Nape alikwenda na kuwa mbele kama nani? Nape ni Waziri kijana. Bado ana nafasi ya kujirekebisha na kjiimarisha. Kujiweka mbelembele kichama ni kuruhusu propaganda za kichama kumuongoza na hata kumuharibia.
Nape, kindly desist yourself from party's events as a central figure. You are now a Minister!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam