figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo NAPE NNAUYE ameliagiza Shirika la Utangazaji nchini -TBC kupima maeneo yake yote yanayomilikiwa na shirika
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo NAPE NNAUYE
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo NAPE NNAUYE ameliagiza Shirika la Utangazaji nchini -TBC kupima maeneo yake yote yanayomilikiwa na shirika hilo ili kuwa na hati zitakazotambulika kisheria ya kumiliki ardhi kwa lengo la kupata wawekezaji kwa maendeleo ya shirika.
Ametoa agizo hilo alipotembelea Kituo cha TBC Kanda ya Kusini LINDI kujionea hali halisi ya jengo la studio ambalo hali yake inatishia usalama wa watumishi wa kituo hicho ambacho kimesimamisha matangazo ya Kanda ya Kusini zaidi ya mwaka mmoja kutokana na uchakavu wa jengo hilo.
Waziri NAPE pia alizungumza na wafanyakazi wa kituo hicho cha TBC Kanda ya Kusini LINDI na kuhaidi kuwa yote waliyomweleza atakwenda kuyafanyia kazi.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kusini JUMA SABIHI ameshauri kuwa kutokana na hali ya Jengo la studio Kanda ya Kusini ilivyo ni vyema shirika likachukua hatua ya kulibomoa jengo hilo kwa utaratibu badala ya kusubiri libomoke lenyewe na kuleta madhara makubwa.
na IBRAHIM UTEGELE