Waziri mwenye mke mtukanaji wajibika

Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Mar 23, 2016
2,624
3,653
Habari ya mke wa waziri aliye mtukana askari polisi akitimiza majukumu yake ndio niyamoto bado.Viongozi wetu hebu jifunzeni kuwajibika wanapokosa waliopochini yenu.
Nikwanini mh.Mahiga angalau usiombe radhi kwa watanzania kwaniaba ya mke wako?Au hajaona wenzake wakiwajibika kwa makosa ya walio chini yao?

Najiuliza pia je huyo mama amewajibishwa kwa kutukana?kama hajapelekwa mahakamani basi apelekwe mahakamani maana ameitukana jamhuri kwa kumtukana polisi.Raisi kuagiza askari aliyetukanwa apandishwe cheo nimatusi makubwa mno kwa familia ya waziri huyo na kama alikua hajajua aelewe kuanzia sasa
Bali ninasisitiza huyo mama afunguliwe mashtaka kwani sheria ni msumeno
 
Mkuu nijuavo mm ukimtukana askari akiwa amevaa kofia yenye nembo ya bibi na bwana hapo hujamtukana yeye Bali umeitukana Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...zaidi ya hyo kwa vile huyo mama alimtukana huyo askari hadharani na kutukana hadharani ni kosa kisheria basi ilitakiwa huyo mama awe ameshafikishwa mahakamani muda huu ninapoandika hii comment. Ila kwa vile ni mke wa waziri rais amesema askari aliyetukanwa apandishwe cheo...ila nadhani rais watuangesema Jamhuri ipandishwe cheo kwani ndo ilitukanwa. Cha pili labda ajafikishwa mbele ya sheria kwa vile ni mke wa waziri. Hv angekuwa ni mke wa mlala hoi sijui ingekuweje.???
 
Kwa hiyo askari akiwa katika sare zake akitukanwa hadharani na vigogo na wanafamilia wao inakuwa neema kwake kwa sababu atapandishwa cheo? Kwa mtindo huo mbona askari wengi watatamani kutukanwa hadharani na hao wakubwa ili wapande vyeo. Na je askari huyo akitukanwa na "malofa" zawadi ya serikali kwa huyo askari ni ipi?
 
Unaongea pumba tupu!!..... Una uelewa kuhusu makosa ya jinai kweli??? Yaani kosa atende huyu(mke wa mahiga) halafu kuwajibishwa awajibishwe mtu mwingine(mahiga)????
 
Pia unao ushahidi gani kuwa alitukana kweli? Je unajuaje kama askali baada ya kuona kanyang'anyana funguo (ambayo kisheria ni kosa, mama anaweza kusema alinyanyaswa kijinsia au alimbaka-si unajua sheria za ubakaji), yaani askali wajifunze jinsi ya kutekeleza majukumu yao.
 
Huko Matusi ni kawaida kama viongozi wao wanatukana watu Malofa unategemea nini kwa wake zao,juzi naibu spika kamtolea maneno yasiyofaa mbunge wa Lindi kwamba aache Ubwege wake, sasa ni mwendelezo wa lugha zisizofaa na tabia ya kiburi cha watu fulani dhidi ya wengine wakumbuke hakuna aliye juu ya sheria.
 
Habari ya mke wa waziri aliye mtukana askari polisi akitimiza majukumu yake ndio niyamoto bado.Viongozi wetu hebu jifunzeni kuwajibika wanapokosa waliopochini yenu.
Nikwanini mh.Mahiga angalau usiombe radhi kwa watanzania kwaniaba ya mke wako?Au hajaona wenzake wakiwajibika kwa makosa ya walio chini yao?

Najiuliza pia je huyo mama amewajibishwa kwa kutukana?kama hajapelekwa mahakamani basi apelekwe mahakamani maana ameitukana jamhuri kwa kumtukana polisi.Raisi kuagiza askari aliyetukanwa apandishwe cheo nimatusi makubwa mno kwa familia ya waziri huyo na kama alikua hajajua aelewe kuanzia sasa
Bali ninasisitiza huyo mama afunguliwe mashtaka kwani sheria ni msumeno

jamani kama hakuna ubaya tunaomba kujua ni mke wa waziri gani aliyehusika na kutukana, na ilikuwa katika situation gani?
 
Hawa watu wenye nyadhifa Serikali na Familia zao somwtimes wanajionaga ni Miungu watu...Siku moja nakumbuka gari yangu ilgongwa kwa nyuma tukiwa kwenye folen..Alie nigonga akataka kujifanya m-babe na yeye ndiyo mweye makosa...Nilimzingua mbaya kabisa kidogo nimkate vibao na kisuti suti chake eti baadae akaniambia wewe unanijua mimi ni Mkuu wa Wilaya ya .....Asee hasira ilizidi kunipmba nikamwambia kwa hiyo ndiyo maana ulitaka kuninyanyasa kisa we ni mkuu wa wilaya/ Nilikomaa nae pale hadi traffic wanafika tukawa akawa ameshanipa Cash yangu ya kutosha kabisa kwenda kushughulikia gari yangu..Ila kwa jinsi alivyokuja angekutana na mtu mwoga angemnyanyasa sana..Hawa watu wanajisahau sana kumbe cheo ni dhamana tu..
 
Kwa hiyo askari akiwa katika sare zake akitukanwa hadharani na vigogo na wanafamilia wao inakuwa neema kwake kwa sababu atapandishwa cheo? Kwa mtindo huo mbona askari wengi watatamani kutukanwa hadharani na hao wakubwa ili wapande vyeo. Na je askari huyo akitukanwa na "malofa" zawadi ya serikali kwa huyo askari ni ipi?
mkuu,usijaribu!bado tunakuhitaji uku mtaani!ebu funika kombe...
 
Pia unao ushahidi gani kuwa alitukana kweli? Je unajuaje kama askali baada ya kuona kanyang'anyana funguo (ambayo kisheria ni kosa, mama anaweza kusema alinyanyaswa kijinsia au alimbaka-si unajua sheria za ubakaji), yaani askali wajifunze jinsi ya kutekeleza majukumu yao.
Tanzania sio kosa kisheria my friend...na ukimpeleka mahakamani unaweza ukabaki humo wewe.

Anakunyang'anya funguo si kwa sababu anapend bali kwa sababu hatuna system itakayowezesha kukutrack hata kama hutaliendesha ilo gari tena.

Alternatively, alitakiwa akuachie uende kisha alipige risasi tairi ili kukuzuia usiondoke.

Mawazo yangu nic askari hawezi kukunyang'nya tu funguo kama hujatishia kuondoka/kutoroka au kubishana naye.

Baada ya kusema haya tuendelee na hoa iliyopo mezani.
 
Ndiyo maana nawachukia sana traffic
 
kweli wewe ni mentor,asante kwa elimu hii mkuu!
 
Hapo ndipo mnapoona dauble standard ya magufuli kwa kuwa ni Mike wa waziri kampa onyo waziri ingekuwa mtumishi wa umma siku nyingi.hii inaitwa aliyetumiwa massage kafukuzwa aliyetuma mpka leo bado ni waziri.Niombeeni sitawaangusha'msema kweli mpenzi sa Mungu(High level of hypocrite never se en)
 
huo upuuz uishie Dar. huku mikoani watu hawarembi mwandiko. kwangua gari ya mtu uone kama hawajakiwasha moto kigari chako.
 
Katika mawaziri wa serikali hii ya rais JPM, balozi Mahiga ni habari nyingine, kuwajibika kwa kosa la mkewe ni upuuzi kwani hakumtuma mkewe ajibuzane na polisi huyo.
 
Back
Top Bottom