Waziri mwakyusa"ajiuzulu" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri mwakyusa"ajiuzulu"

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Sep 1, 2008.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,627
  Likes Received: 5,790
  Trophy Points: 280
  MKUU ACHA KUCHEZA NA MAISHA YA WATU HUU SI UTAWALA WA KIFALME KAMA UNAVYODAI UKIJIUZULU UTAFUTIWE MBADALA WEWE UNAWEZA KUTAFUTA MBADAKA NA MAITI ZA WATOTO WASIO NA HATIA WALIOATHIRIKA NA CHANJO,,,ACHA MCHEZO MZEE SUGUA WAACHIE WENGINE WEWE KABLA YA KUWA WAZIRI KUNA MTU ALIMPELEKEA JINA LAKO RAISI??????????NDIO AKATOLEWA ALIEKUWEPO!!1MBONA MNAJIBU MASWALA KAMA HAMJASOMA JAMANI SHULE HANI HIZI???????????HAYA

  Mwakyusa:Natafakari ushauri wa kujiuzulu


  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa, amesema ushauri wa kutakiwa kujiuzulu kufuatia matatizo yaliyojitokeza ya watoto kuzirai baada ya kupewa dawa za chanjo ya kichocho na minyoo, amelipokea, lakini bado anautafakari.

  Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, Profesa Mwakyusa alisema ndio kwanza ameingia jijini Dar es Salaam akitokea safarini, hivyo suala la yeye kutakiwa ajiuzulu ndio kwanza amelisikia.

  ``Sasa siwezi kutoa jibu kwa haraka, suala la kujiuzulu ni kubwa, bado ningali nafikiria,`` alisema.

  Hata hivyo, waziri huyo alisema hatochukua hatua ya kujiuzulu kwa pupa au kwa lengo la kumfurahisha mtu mmoja.

  Kuhusu madhara ya dawa hizo, alionyesha kushangazwa na watu `kuvalia njuga\' matatizo `machache` yaliyotokea, bila hata kutaka ufafanuzi wa Serikali.

  Profesa Mwakyusa alikanusha madai kwamba, palikuwepo na ufisadi katika uingizwaji wa dawa hizo kama ilivyodaiwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Fellowship, Zakaria Kakobe.

  Waziri Mwakyusa alisema wanaotoa tuhuma hizo hawafahamu na bila shaka wanahisi tu bila kuwa na ushahidi na kuongeza kuwa tatizo hilo linaweza na kuonekana kubwa kuliko uhalisi wake.

  Alisema hakuna mtu ndani ya wizara yake anayeweza kuwa na wazo la kuhujumu afya za wananchi. ``Hawa wanaosema hivyo, nafikiri wanadhani tu,`` alisema Profesa Mwakyusa.

  Waziri huyo alisema wakati anatafakari suala la kujiuzulu, wanaomtaka afanye hivyo, ni vema pia wamtaje mtu ambaye wanaona anafaa kuwa Waziri wa Afya badala yake.

  ``Kama mimi wanaona sifai sawa, lakini pia wanatakiwa wamtaje kwamba nani wanadhani anafaa zaidi yangu, wamtaje huyo mtu ili na Rais anayeteua mawaziri alione jina hilo,`` alisema.

  Alipotakiwa atoe ufafanuzi kama suala la kujiuzulu atalitafakari kwa muda gani, waziri huyo alisema hafahamu.

  Juzi, Askofu Kakobe alikaririwa akimtaka Profesa Mwakyusa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Willison Mkama wajiuzulu mara moja kutokana na tukio hilo.

  Askofu Kakobe alisema watendaji hao wa Serikali na walio chini yao, walipaswa kuhakikisha kwamba dawa hizo za chanjo hazina madhara kwa binadamu.

  Wakati huo huo, Fitina Haule wa PST anaripoti kutoka Morogoro kwamba Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) imetuma wataalam wake mkoani Morogoro kutathmini ubora wa dawa na madhara yaliyojitokeza kufuatia zoezi la chanjo ya vitamin `A` na utoaji madawa ya minyoo na kichocho.

  Inadaiwa kuwa zaidi ya watoto 300 wa shule mbalimbali za msingi waliathirika na dawa hizo.

  Timu ya watu wawili wakiongozwa na Kaimu Mkurungenzi wa Mamlaka hiyo, Bw. Hiiti Sillo ilifika mkoani hapa juzi kwa lengo la kufanya utafiti ili kutaka kujua kama madhara yaliyojitokeza kwa watoto hao yanahusiana na kusababishwa na dawa walizopewa au kuna mengine.

  Bw. Siilo alisema watatafiti kwa undani zaidi ili kubaini ukweli wa madhara hayo ya dawa kama inavyodaiwa, sambamba na kubaini kama upo uhusiano wa madhara na ubora wa dawa.

  Alisema, wamelazimika kuja wenyewe mkoani hapa na kufanya utafiti huo kwa muda wa siku tatu baada ya kuona na kusikia kupitia vyombo vya habari madhara yaliyotokea katika chanjo hiyo.

  Alisema baada ya utafiti huo na kama watajua kuwa dawa hizo zinahusika na madhara hayo, watawasiliana na watayarishaji wa madawa hayo ili waweke alama zinazofafanua juu ya madhara ya dawa hizo ambapo itasaidia mlengwa kutambua matokeo ya dawa hizo kabla hajayanywa.

  Naye Mbunge wa jimbo la Morogoro, Dk. Omari Mzeru Nibuka ambaye ana taaluma ya udaktari wa binadamu alisema kuwa utaratibu mzima wa utoaji wa chanjo hiyo ulikuwa na mapungufu mengi.

  Akizungumza wakati alipotembelea Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, aliyataja mapungufu hayo kuwa ni pamoja na kugawa dawa aina mbili kwa wakati mmoja.

  Mapungufu mengine alisema ni kutowapa chakula kwa wakati watoto kulingana na masharti ya dawa na kutotoa elimu ya kutosha kwa wazazi juu ya athari za dawa hizo.
   
 2. C

  Chuma JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hii kesi Kubwa....naona imekosa atension kwakuwa ipo Huku porini..MODs please ipeleke ktk Siasa then ijadiliwe....

  Binafsi niliona hio, ikabidi mke wangu nae aniarifu kuwa amestopisha kumpeleka mtoto wetu huko....kwa hali watoto wote walipwe FIDIA... na Waziri husika Ajiuzulu..suala la kesema eti watu wamataje nani awe next baada yake ni uchovu wa kufikiri..kwanza si Jukumu la wananchi...
   
Loading...