Waziri Mwakyembe tunahitaji huruma yako TAA

Waziri Mwakyembe tunahitaji huruma yako TAA

FIRE TENDER

Member
Joined
Sep 7, 2012
Posts
15
Reaction score
1
Nashindwa kuelewa sijui kwanini waziri Mwakyembe unashindwa kuchukua hatua kwa madudu yanayoendelea ndani ya mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania( TAA),sababu ni taasisi inayoendeshwa kihuni sana kama genge la wahuni wachache.

Hii pia ni moja ya taasisi iliyo chini yako, kwa kukusaidia chunguza yafuatayo:

Undugu katika upandishaji wa vyeo

Kuminya nafasi za kusoma kwa watumishi wenye sifa: wale wenye god fathers are the ones who enjoy fruits of this agency. kuna watumishi wanazaid ya miaka kumi kazini lakini wakiomba kwenda kusoma wanatishwa katika ruhusa zao mfano mtu unaambiwa utarud kazin ikiwa nafasi yako bado ipo, hiyo imekuwa inawatisha watumishi wengi kutokwenda kusoma kwa hofu ya kupoteza ajira.

Wakuu wengi wana elimu ndogo sana,hiyo inapelekea utendaji wao kuwa mbovu kuliko maelezo lakini wamekuwa wakilindana. ni aibu kwa mamlaka kubwa kama hii kuwa na wakuu wenye elimu ya kidato cha nne,hii hali imepelekea wale watumishi wa kawaida wenye elimu ya juu kupigwa mizengwe mara kwa mara kwa kuwa wanaonekana kuwa threats kwa wakuu wao.

Wakati watumishi wa kawaida wakibaniwa nafasi hata za kusoma vyuo vya ndani kwa ngazi mablimabali, wakuu wamekuwa busy kupeana trips za nje zisizo na tija kwa mamlaka, mfano kuna meneja wa kiwanja flan alipelekwa nje wakati amebakiza miezi isiyozid mitano kustaafu,chunguza hili utapa majibu kwani ni moja ya ishu iliyowakera watu wengi sana.

Trainnig zimekuwa adim kwa wafanya kazi,hii imepelekea watu kufanya kazi kwa kubahatisha,hii ni aibu kwani hii ni sekta muhimu na yenye kuhitaji watumishi competent ndo maana katika nchi mbalimbali wakiwemo jirani zetu wamekuwa wakijitahid sana kusomesha watumishi wa sekta hii.

Huku kwetu hata kuwekwa kwenye program ya kwenda katika mafunzo inatakiwa uwe na mtu au ukubali kugawana mshiko na mpiga debe. In short kila kitu ni deal huku,mambo hayaendi bila kutangaza dau au kuwa na god father.

Kuna madudu mengi sana katika mamlaka hii ambayo yanahitaji muda mwingi kuyaelezea hila kwa leo ngoja nihishie hapo lkn pia chukunguza watoto wa vigogo kupewa ajira sehemu mbalimbali ikiwemo makao makuu ya TAA bila kufuata taratibu,(hazitangazwi wala hawafanyiwi usaili) wamejaa wengi sana wanawapa mikataba ya mwaka which is renewable mpaka pale watakapo pata ajira sehemu zingine.

Kwa kuwa sasa imekuwa ngumu kuwaingiza katika system kutokana na ajira kupitia tume ya ajira.
 
Back
Top Bottom