Waziri Mwakyembe amebadili gia angani?

Nyerere alituasa na kutuhamasisha kwamba 'SIASA NI KILIMO', tena ni azimio la Iringa mwaka 1972. Kwa hiyo yeye Mwakyembe hataki KILIMO na kama ni hivyo Mwakyembe hawataki watanzania kwa asilimia 80%. Maana tunaambiwa 80% ya watanzania ni wakulima.
 
Hivi elimu yote aliyonayo mwakyembe hawezi kuendesha maisha nje ya uwaziri mpaka afikie hatua ya kufanya siasa zenye kumdhalilisha kiasi hiki!!? Hivi kuna faida gani ya kuelimika ikiwa msomi kama huyu anakubali vitu ambavyo hata asiyesoma hakubaliani navyo!!?
 
Katumwa aseme hivyo, ili mkuu aje aitengue hiyo kauli kama alivyofanya kipindi kile cha bila vyeti vya kuzaliwa hakuna kufunga ndoa.
 

kipindi kile alikuwa anatafuta kikiiiii
 
uzee unamsumbua,wenzake washastaafu na heshima zao lakin yeye ulafi wa madaraka ndio chachu ya yeye kuwepo hadi leo
 
wasanii wasipoingia kwenye siasa, Nchi itakuwa imepiga maendeleo sana.Ila wanatumika pote tu ingawa hata US tuliwaona wasanii wako upande wa mama Hilary ila kwetu wamezidi
Kila mmoja afanye kazi zake.
kazi zao ni kuimba, waimbe nini tuwaachie wao. Upande unaoongoza kuwatumia wanamuziki ni serikali na CCM. Tatizo wao wakiwatumia wanamuziki 30 sio tatizo ila upande fulani ukiwatumia wawili tu ni tatizo. Huku ni kutojiamini kwa kiwango cha PhD.
 
kama wanamuziki wakikatazwa kuimba nyimbo za maudhui ya siasa, CCM na serikali ndio itakayoathirika zaidi. Tunaona kwenye sherehe za serikali na mikutano ya kampeni ya CCM, bila kujaza wanamuziki haifani so katazo hili ni hasara kwao kuliko faida
 
wasanii wasipoingia kwenye siasa, Nchi itakuwa imepiga maendeleo sana.Ila wanatumika pote tu ingawa hata US tuliwaona wasanii wako upande wa mama Hilary ila kwetu wamezidi
Kila mmoja afanye kazi zake.

Wewe una akili halisi ama ya kugushi, kazi ya mwanamuziki ni kuimba anachoona kina maslahi kwake! Tatizo ni kwamba watu hawapendi kusikia jinsi upande wa pili unavyowatathmini!!! Shame on you
 
Mimi ninafikiri tatizo halianzii kwa huyu ndugu Mwakinembe, bali ni upotoshwaji na ukengeushi tena wa makusudi wa dhana nzima ya SIASA ambao umeasisiwa na mkuu wa kaya. Kuna haja ya wanazuoni na wananchi wa Tanzania kuwa na mjadala uliomakinika kuhusu dhana ya SIASA na tukubaliane 'SIASA' ni nini? Mkuu wa kaya amepiga marufuku vyama vya siasa kufanya 'siasa' hadi 2020 lakini tunaona Chama cha Mapinduzi na yeye pia kwa kofia ya Rais na Mwenyekiti wanafanya 'siasa' kama kawa! Sasa na ndugu Mwakiembe naye anakuja na fikira hizo hizo kuwa wanasanii wasiimbe 'siasa' (pengine naye anamaanisha hadi 2020!).
 
Maana nzima ya kile anachokisema Mh Mwakyembe unakipata kupitia mifano yake ya wanamuziki aliowataja. Nyimbo za kisiasa alizozikataza ni zile zenye kuibua mgogoro kati ya serikali na mwanamuziki. Hapa alitoa mfano wa Fela Ramson Anikulapo Kuti wa Nigeria kuimba nyimbo za kushambulia wanasiasa zilimfanya afe kama chokolaa.
Kwa yeyote mwenye akili, sijui hapa nikikujumisha nitakuwa nimekosea,anafahamu kuwa Mh Mwakyembe hajazuia Mwanamuziki kuimba nyimbo za kuumpa shime,kumuasa na kumkumbusha mwanasiasa,chama na wananchi juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea katika jamii bila nia ya kutweza.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…