Waziri Muhongo tuondolee tatizo la umeme Lindi na Mtwara

Mkulia

JF-Expert Member
Apr 26, 2012
375
95
Licha ya kuwa na vyanzo vya uhakika vya uzalishaji wa nishati ya umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara bado tatizo la upatikanaji wa huduma hiyo ni kubwa.
Kwa ujumla upatikanaji wa umeme katika baadhi ya maeneo ya mikoa hii hususa katika wilaya za Masasi, Nanyumbu,Newala na Nachingwea siyo wa uhakika. Tangu msimu wa kiangazi hadi sasa umeme hupatikana kwa shida kubwa sana. Mathalani katika Siku moja (saa 24) umeme unaweza kupatikana kwa saa 5 hadi saa 8 tu au usipatikane kabisa. Cha kushangaza viongozi wa TANESCO hawawaelezi wananchi chanzo cha matatizo hayo na yatadumu kwa muda gani.
Hivyo,tunakuomba waziri Muhongo uingilie kati tatizo hili kwani limeanza kuwa sugu na ikibidi fanya ziara ya kikazi katika maeneo tajwa.
 
Ameanzia mabwawani kwanza, natumaini siku si nyingi atakuja visimani.
 
Back
Top Bottom