Deo Corleone
JF-Expert Member
- Jun 29, 2011
- 17,005
- 13,271
Wizara ya Nishati na Madini,imewaita wawekezaji wazawa kuwekeza kwenye uzalishaji wa umeme kupitia vyanzo vifuatavyo.
Gesi asilia
Makaa ya mawe
Umeme wa Maji.
Biogas
Na umeme wa upepo.
=========================
Chanzo: Mwananchi
Gesi asilia
Makaa ya mawe
Umeme wa Maji.
Biogas
Na umeme wa upepo.
=========================
Dar es Salaam. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amewataka wawekezaji wa ndani wenye uwezo wa kuwekeza kwenye umeme, kujitokeza kuwania zabuni za kusambaza nishati hiyo.
Kauli ya Profesa Muhongo imekuja wakati akilaumiwa kwa madai ya kubagua wazawa kwenye uwekezaji wa vitalu vya gesi na mafuta kutokana na kauli yake kuwa hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kifedha kuweza kufanya kazi kwenye sekta hiyo.
Jana alitoa nafasi hiyo kwa wawekezaji wa ndani kuchangamkia eneo hilo ili kuleta mabadiliko katika kuimarisha usambazaji wa nishati hiyo muhimu.
Muhongo, akiwa ameongozana na katibu mkuu wa wizara hiyo, Mhandisi Omary Chambo na Naibu Waziri Medard Kalemani, alitoa wito huo alipoongea na waandishi wa habari baada ya kufanya kikao na wafanyakazi kwenye ofisi za makao makuu ya Tanesco.
Akijibu swali kuhusu ununuzi wa nguzo za umeme nje ya nchi badala ya kutumia zinazozalishwa na kampuni za ndani, Profesa alisema awali waliamini Watanzania wana uwezo wa kuzalisha nguzo za kutosha, lakini baadaye wakabaini kuwa si kweli.
Alisema mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini (REA) kuhitaji nguzo nyingi na hivyo zinazozalishwa nchini hazitoshelezi mahitaji ya mradi huo.
Profesa Muhongo aliingia kwenye mgogoro na wafanyabiashara wa ndani kuhusu vitalu vya gesi na mafuta kutokana na kauli yake kwamba sekta hiyo inahitaji uwekezaji mkubwa wa kifedha na hivyo ni vigumu kwa wazawa kuingiza. Kilichowaudhi zaidi wazawa ni kauli yake kwamba wanaodai kubaguliwa ni madalali wa makampuni ya nje. Na suala hilo lilipoibuka bungeni wakati wa kashfa ya uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, Profesa Muhongo aliwaelezea wabunge waliopaza sauti zao kutetea wazawa kuwa wanafanya marejesho ya fedha walizopewa na wafanyabiashara kwa kuzungumzia suala hilo bungeni.
Mbali na kutoa nafasi kwa wazawa, Profesa Muhongo aliagiza watumishi wote wa mashirika ya wizara hiyo kuhakikisha tatizo la kukatika mara kwa mara kwa umeme likome ifikapo Februari mwakani, na endapo itashindikana viongozi wa Shirika la Umeme (Tanesco) watawajibishwa.
Katika hatua nyingine, kaimu naibu mkurugenzi mtendaji wa usambaji umeme wa Tanesco, Mhandisi Sophia Mgonja amesema wameanzisha utaratibu mpya utakaowasaidia wateja wa shirika hilo kuwasiliana moja kwa moja na maofisa wawili ndani ya ofisi ya dharura nchi nzima.
Mhandisi Mgonja alisema katika kila ofisi ya kitengo cha dharura kutakuwa na ofisa wa huduma kwa wateja na mhandisi mmoja ambao watasimamia muda na ubora wa huduma wanazopata wateja baada ya kutoa taarifa za dharura.
Chanzo: Mwananchi