Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Kwanza nikiri Waziri Mpango (Waziri wa wetu wa Fedha) ni mmoja kati ya Mawaziri ninaowakubali sana na nina uhakika kama wakienda vizuri na Raisi Magufuli basi hakika TanZania mpya na ya yenye uchumi uliosimama na unaojitigemea haiko mbali sana!
Nampongeza sana Waziri Mpango kwa jitihada zake kubwa za ukusanyaji wa kodi na kutuonyesha matumizi ya fedha zetu kila mwezi!
Sasa hivi ni dhahiri kwamba karibia kila Mtz anabanwa kulipa kodi ambapo ni sawa lkn pmj na hayo kuna hili swala la wenye Nyumba ambao kwangu mimi hapo kuna fedha nyingi sana inavunwa na wenye hizi nyumba bila kukatwa kodi au wanakatwa kodi ndogo sana aambayo haiendani na thamani ya nyumba zao!
Nitatoa mfano kuna nyumba nyingi sana maeneo ya Masaki, O'bay, Upanga, Msasani au hata Kinondoni ambapo watu wanalipia kodi ya nyumba mpaka dola (US) 4000 kwa mwezi na nyumba hizi ziko nyingi sana, mapartment yote yaliyoko Upanga ya Wahindi na Wanasiasa wa zamami wanakula hela ndefu ktk kwa Wapangaji bila kulipia kodi au kwa kulipia kodi ndogo ambayo haindenani na wanachovuna!
Kuna watu wanauza viwanja mpaka milioni 500 lkn hawalipi au wanalipa kodi kidogo sana, wengine wanamiliki nyumba ya thamani ya kuanzia milioni 100 na kuendelea lkn analipa shilingi 50 000 (efu hamsini) tu kwa mwaka!
Haya ni mapato makubwa sana, Mji wetu wa Dar ndiyo moja kati ya miji aghali sana kupanga ofisi Duniani, kukodisha kwa Ofisi /m² Dar yetu ni sawa au aghali klk New York (USA) na Ofisi zimejaa lkn nina uhakika hawa wenye ma skyscraper hawalipi kodi yetu kulingana fedha wanayochukuwa!
Hivyo wito wangu najua wewe ni Intelligent man na sipaswi kukupa ushauri kama huu kwani ni lazima wewe mwenyewe umeshaliona hili na labda utekelezaji wake ndiyo una changamoto lkn ningependela kama vile Wafanyabiashara wanavyopewa EFD basi na hawa wenye maskyscraper pia wapewe EFD ili kila mwezi walipe kulingana na kodi wanazotoza!
Chukulia Mwanasiasa kama Lowasa, anamiliki Jengo lililokodishwa na Ubalozi wa AK Masaki, sasa sidhani kama kweli fedha ya kodi anayolipwa Lowasa kwa mwezi analipia VAT au hata kama analipa kodi kulingana na thamani ya jengo na eneo, hivyo ningeshauri watu kama Ubalozi wa AK wapewe EFD na kila kodi wanayomlipia Lowasa kwa mwezi au mwaka asilimia fulani iingie Serikalini lkn huwo ni mfano tu wa jinsi tunavyopoteza fedha nyingi sana, kwani matajiri haswa hawalipi au wanalipa kidogo sana lkn wananchi wa kawaida ndiyo tunakatwa moja kwa moja kwenye mshahara hapo hatukwepi!