Waziri mkuu wa Serbia ahamishiwa mahala salama

amygdala

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
1,082
997
_92150972_aleksandarvucic.jpg


Maafisa wa polisi huko Serbia, wamemuondosha waziri mkuu wa nchi hiyo Aleksandar Vucic na familia yake, hadi maeneo salama, baada ya kupatikana kwa idadi kubwa ya silaha karibu na nyumbani kwake, kilomita kadhaa kutoka mji mkuu Belgrade.

Ugunduzi wa silaha hizo zikiwemo bunduki hatari za kurusha maroketi, magruedi yanayorushwa kwa mkono na makasha kadhaa ya risasi.

Waziri wa maswala ya ndani ya taifa hilo, Nebojsa Stefanovich, amesema kwamba silaha hizo zilipatikana karibu na njia panda mahali ambapo gari la waziri mkuu huwa inapunguza mwendo kabla ya kufika nyumbani kwake.
_92150974_nebojsastefanovich.jpg


Bwana Vuchich zamani alikuwa mwanamapinduzi na mwanaharakati mkubwa aliyekuwa akishinikiza kwa mataifa iliyokuwa muungano wa Usovieti kurejea pamoja na kuunda muungano huo, Lakini alibadilisha kauli yake na kuunga mkono ujumuishwaji wa mataifa hayo ndani ya muungano wa EU.

Polisi bado hawajamtia mbaroni mtu au kundi la watu wanaohusishwa na upatikanaji huo wa silaha.

Bado kungali na mamia kwa maelfu ya silaha haramu nchini Serbia, iliyoachwa wakati wa vita vya Yugoslavia vya miaka ya 1990
Waziri mkuu wa Serbia ahamishiwa mahala salama - BBC Swahili
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom