Waziri Mkuu wa Myanmar kutoa ushahidi katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,116
Waziri Mkuu wa Myanmar Aung San Suu Kyi atatoa ushahidi leo katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu. Serikali ya nchi hiyo iliyo kusini mashariki mwa Asia inadaiwa kupanga mauaji ya halaiki ya Waislamu walio wachache nchini humo Warohingya.

Mwaka 2017 maelfu ya Warohingya walikimbilia nchi jirani ya Bangladesh baada ya mashambulizi ya polisi na wanajeshi yaliyoitikisa nchi hiyo.

Aung San Suu Kyi ambaye alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1991 amekosolewa pakubwa kutokana na kuchelewa kwake kuzungumzia udhalimu huo.

Mahakama ya Juu ya Umoja wa Mataifa ilifungua kesi dhidi ya serikali ya Myanmar baada ya serikali ya Gambia kuweka shinikizo.
 
hapo panaweza kuwepo makosa ya crimes against humanity na genocide. download kitabu hiki kipo kwa kiswahili kueleza ICC na jinsi inavyoshughulikia mashitaka yake.
 

Attachments

  • MAHAKAMA YA ICC - THE HAGUE.pdf
    1,019.2 KB · Views: 1
Back
Top Bottom