Waziri Mkuu: Sakata la Ben Saanane, ipeni muda serikali ifanye kazi

utaifakwanza

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
14,193
2,812
Akijibu swali la kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, waziri mkuu kassim majaliwa amesema kuwa serikali imesikia na ipewe muda ifanye kazi. Ifanyie kazi suala la beni sanane na kukomesha matukio yote ya aina hiyo. Majaliwa amesema serikali iko macho na inalaani kwa nguvu zake zote unyama huo na inawasihi wananchi kushirikiana na dola kupata taarifa za kufankisha kupatikana kwa beni
 
Attachments

  • tmp_27836-IMG-20170420-WA00251979134764.jpg
    tmp_27836-IMG-20170420-WA00251979134764.jpg
    63.7 KB · Views: 67
Akijibu swali la kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, waziri mkuu kassim majaliwa amesema kuwa serikali imesikia na ipewe muda ifanye kazi. Ifanyie kazi suala la beni sanane na kukomesha matukio yote ya aina hiyo. Majaliwa amesema serikali iko macho na inalaani kwa nguvu zake zote unyama huo na inawasihi wananchi kushirikiana na dola kupata taarifa za kufankisha kupatikana kwa beni
Sidhani, sidhani, sidhani kama kuna nia ya dhati.
Mawsiliano yapo wanaweza kuyatrace last maongezi ya Ben quite simply, why there is inertia in pursuing this! .... jaribu kutuma neno baya kuhusu nchi kwa simu uone, utafikiwa baada ta dakika zisizozidi 10! Why inertia on this?
 
Ndugu Kassimu nae kaelemewa..Juzi niliposoma lile andiko la yule kijana wa cdm aliyekuwa akiteswa na kuvutwa pumbu na Polisi wa kike nilihudhunika sana.Inawezekana Usalama wa taifa wala hawahusiki ni hawa hawa policcm ndio wahusika
 
Rekebisha maneno yako
 
Jibu zuri, sasa yoyote mwenye habari awapelekee kama alikuwa ameikalia kimya. Hata kidunchu ha info kinaweza kusaidia sana sana kujua ukweli wa kilijlchojiri

Kingine waanze na waliokuwa wamemuajiri, wanaishinda nae au kuonana nae kila siku kama wapo. Je walilipoti polisi walipoona mfanyakazi wao hajatokea kazini? Au waliwauliza ndugu zao? Baada ya muda gani? Na nani alienda kutoa taarifa kuwa kapotea na alisema kwa sababu gani? Je kuna wengine wakaribu na awaliokuwa karibu nae wanaweza kujua lolote? Kila mtu mara ya mwisho kumuoma alikuwa amevaaje na rangi ya shati etc..
Kuna aliyeongea nae kabla hajatoweka? Passport yake kama anayo ipo kwake au? Pesa benki zimetolewa baada au ni kabla hajapotea tu? Kuna malipo ya ajabu au pesa kutoka kwake kurushwa kwingine ambazo hazijakaa kikawaida? Bila kusahau ndugu zake inabidi wakumbuke maneno yoyite akiyaongea ambayo sasa hivi wataona yanakitu ndani yake au watu aliowatajataja. Na mengine mengi
 
Serikali na wananchi ni wadau muhimu katika hili. Chadema ambayo beni ni mfanyakazi wake pia ina la kutuambia
 
sijaelewa vizuri hii kauli "ametangulia mbele ya haki au amepotea"

to be specific kasema hivi "familia ya mtajwa, aliyetutangulia mbele ya haki au vinginevyo, hata sina uhakika"
 
Kila mwenye taarifa za uhakika bila kujali itikadi au chuki binafsi atoe ushirikiano
 
Tumwoneeni huruma PM, ukimtizama kwa umakini utagundua kuna mambo yanaendelea hakubaliani nayo, lakini sasa afanyeje? Yote kwa yote ni ujima mwananchi maarufu kama Ben Saanane kutekwa kwa sababu ambazo wote hapa tunazijua
 
Kauli tata 'ametangulia mbele za hali au vinginevyo Sina uhakika'
 
Back
Top Bottom