Waziri Mkuu Majaliwa: Madhara Ya SCT Kiuchumi-Mapato Ya Bandari Yameshuka

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
1,169
1,073
MFUMO WA PAMOJA WA FORODHA{SINGLE CUSTOMS TERRITORY} UNASABABISHA MADHARA MAKUBWA HASA YA KIMAPATO KWA BANDARI ZETU HIVYO KUDIDIMIZA JITIHADA ZA NCHI KUJITEGEMEA KATIKA KUSUKUMA KASI YA MAENDELEO KWA KUTUMIA MAPATO YA NDANI.

Nianze kwa kupongeza juhudi za dhati za serikali ya awamu ya tano kufanya utakaso wa uozo mwingi ktk bandari kuu Tanzania.Nipongeze kwa dhati umakini mkubwa wa Waziri Mkuu Mh.Majaliwa na wote wanaompa taarifa nyeti kwa maslahi ya taifa.

Mizigo inayopita katika bandari zetu imepungua sana sana japo takwimu zaweza kufichwa lakini ukweli upo wazi..hivyo mapato yamepungua mno,athari kwa wadau ni kubwa mno,athari kwa sekta ya wawakirishi wa wenye meli...Pamoja na mdororo mdebwedo wa uchumi wa dunia lakini pia mfumo wa SCT ni moja ya sababu.

Tunaihitaji sana nchi ya Congo DR{Serikali,Wafanyabiashara-wadogo kwa wakubwa,wapya kwa wazamani} katika kufanikisha malengo yetu kimapato na kibiashara kwa maslahi ya taifa.

Lazima tukubali kwamba Kuhihusisha Congo DRC ktk mfumo wa utoaji/usafirishaji nje mizigo kupitia bandari za nchi wanachama wa Jumuiya ya Africa Mashariki kuna athari kubwa sana kwa uchumi wa nchi yetu {Tanzania}..Wateja wengi wamekimbia kutumia kutumia bandari zetu ..na ikumbukwe Importers and exporters toka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo wamekuwa wakibeba asilimia kubwa sana ya waagizaji wa nchi jirani wanaopitishia mizigo katika bandari za Tanzania na hata Mombasa {Kenya}.

Zaidi sana hata mizigo mingi iliokuwa inaagizwa na waagizaji wa Nchi za Rwanda na Burundi watumiaji wa mwisho wa bidhaa husika walikuwa ama ni wakongo toka maeneo yanayopakana na nchi husika.

Nini Ubaya wa Single Customs Territory na mfumo wake?

Mfumo unawalazimu waagizaji kuwa na mtaji mkubwa sana kibiashara unaoweza kufanikisha malipo ya ununuzi wa mzigo,usafiri,kodi na gharama zingine huku wakisubiri kwa muda mrefu pasipo mizigo husika kuwafikia.Hili limewafanya wafanyabiashara kubeba mzigo mkubwa hata kufanya biashara husika kuwa kama adhabu,mateso,shida hasa wanapotumia milango bahari ktk nchi zenye mfumo tajwa.

Mfumo unawalazimisha waagizaji toka nchi wanachama wa EAC na nchi waalikwa {Congo DRC} kulipa ushuru na kodi zote kabla mizigo haijatolewa katika bandari hususani ya Dar es salaam hivyo kubeba risks kubwa kibiashara kutokana na udhaifu wa mifumo na miundombinu hasa katika usafirishaji kupitia barabara,wizi,uharibifu.

Ucheweleshaji wa kutoa mizigo unaotokana na mwingiliano wa uhakiki,ufuatiliaji,tathmini,ukaguzi baina ya taasisi au mamlaka za kodi katika nchi ambazo mzigo unapitia/fikia/kombolewa kiforodha.Ucheweleshaji husika hupelekea gharama kuongezeka maradufu hasa ukihusisha tozo za ziada ktk bandari {port charges-removal,storage charges},mamlaka za kodi {Customs warehousing rent} na wamiriki makasha {demmurage charges} kwa mizigo iliohifadhiwa makashani {containerised cargoes}.

Ukosefu wa ushirikiano wa dhati baina ya wadau wa bandari kuu hivyo kupelekea mikwamo ya maamuzi ktk utekeleaji mkakati kwa maslahi ya taifa.Mfano ni uwepo wa wamiriki wa bandari kavu wenye maono ya kupata faida tu wakati wote,popote,vyovyote hapa katika mazingira ambayo wanapaswa kupata hasara kidogo kwa ajili ya mkakati wa makusudi kupata faida kubwa mbeleni.Vivo hivyo ushirikiano baina ya mamlaka za bandari,TRA na mawakala wa forodha..Kumekuwepo na uadui mkubwa na kuwindana badara ya ushirika mtakatifu kwa maslahi ya taifa.Mfano. Bandari wanapomchaji mteja storage charge hapo hapo TRA wanamchaji mteja huyo huyo Customs warehousing rent {equivalent to storage charge though they differ in calculations formula}.

Mapendekezo:
-Serikali ichukue hatua mahsusi za kidiplomasia kwa kupitia upya makubaliano yaliofikiwa kupitia EAC.

-Serikali ifanye tathmini ya kina ya madhara tajwa kwa kupitia ripoti zilizopo TRA/TPA na ikithibitika hasara tajwa isitishe kwa dhalura ushiriki wa nchi ya Congo DR ktk mfumo wa SCT.

-Walioshiriki kupendekeza mapendekezo yenye mapungufu kwa nchi yetu waangaliwe kwa jicho la nne ili iwe fundisho kwa wengine wanaofanya maamuzi yanayoigharimu nchi na vizazi vilivyopo na vijavyo.

-TPA kupitia ofisi yao ya Lubumbashi-Democratic Republic of Congo wawezeshwe kimkakati ili kuwashawishi wateja wengi waliokimbilia katika bandari za nchi jirani zisizo na mfumo wa SCT kama Namibia-Welvis Bay Port,Msumbiji-Beira Port,Afrika Kusini-Durban port na Angola-Lobito Port.

-Serikali ifanye maamuzi ya kuipatia serikali ya Kongo eneo mahsusi kuwa Bandari kavu kwa ajili ya kusaidia kushusha tozo adhabu{ kwa mizigo inayokwenda Kongo} zinazofanya bandari yetu kuwa ghali kibiashara hivyo kudidimiza ustawi kibiashara {vital essence in international trade/Supply chain/International Logistics }.

-Kitengo cha Huduma kwa wateja wa bandari zetu kiimalishwe na kifanye kazi kwa weredi uzalendo na kwa maslahi mapana ya nchi {Great Care and Attention} kwa kuhakikisha wadau wote wa bandari wanatoa huduma za kisasa,ubora,kwa unafuu na kwa haraka sana na si kama ilivyo sasa ambapo Rushwa,wizi,utapeli,uongo,ucheweleshaji,ufinyu wa utoaji taarifa,usumbufu n.k vimekuwa vitu vya kawaida wanavyotuhumiwa navyo sana wafanyakazi wa TPA,TRA,ICD's,Mawakala wa Forodha {CFA}.

-Kutengenezwe Transit informations centres maalumu kwa ajili ya kuwahudumia wateja wa nchi jirani zikiwa na huduma muhimu kuvutia wateja zaidi kurudi tena na tena {kama taarifa za bandari,mawakala,utalii,malazi,barabara,shopping,starehe etc}
 
Dah we utakuwa mzalendo sana, hongera sana kwa uchambuzi makini , big up, nadhani mawazo yako yote yakifanyiwa kazi basi mizigo na mapato yataongezeka
 
Nilianza kwa kudhani Majaliwa ndie kasema maneno haya, kumbe unaelekeza ujumbe wako kwake. Hongera. Umeongea vizuri. Mvurugano uliopo hapo bandarini ni kichefuchefu. Kwa mfano ukiomba port charge kwenye mtandao, kama hukumtumia mtu wa ndani shs 10,000/=, port charge itatoka baada ya siku 3.
 
Dah we utakuwa mzalendo sana, hongera sana kwa uchambuzi makini , big up, nadhani mawazo yako yote yakifanyiwa kazi basi mizigo na mapato yataongezeka

Siwezi kukubali au kukataa kwamba naweza kuwa mzalendo sana..Binadamu tuna mapungufu,dhambi na maovu ya hapa na pale ila rehema za mwenyezi Mungu zatufunika.
 
Tusubiri tusiwe na haraka ya mapato,, acha watu wazoee kwanza then hali itakuwa nzr tu,,

Bora hivi sasa kuliko msururu wa maroli ya Lake Oil ulivyokuwa inasumbua barabarani kumbe ni mafuta ya magumashi,,

Bora tupate kidogo hivi hivi kuliko tulivyokuwa tunaibiwa.
 
Tumia akili usiwahi kuandika utumbo na ushabiki....

Dunia ya sasa inahitaji mapato we unasema bora tupate kidogo? Bandari ya DSM inakimbiwa kila uchao...
 
Nasikia mwaka ujao wa fedha magu anataka bajeti ya Serikali iendeshe na makusanyo ya pesa za ndani tu,hataki misaada
 
Hapa mtawasikiliza watu ambao ni beneficiary wa mfumo wa zamani... ulitakiwa utoe taarifa kisayansi co unaongea tuuuuuuuu
 
Beneficiary wa mfumo wowote ,popote Tanzania,vyovyote ulivyo wanapaswa kuwa watanzania wa leo,kesho na kesho kutwa kwa maana ya vizazi vilivyopo na vijavyo.Niwie radhi ndugu kwa kushindwa kuwa na taarifa za kisayansi sababu ukosefu ya elimu bora ya kuniwezesha kuwa mwanasayansi kiutafiti,kiubunifu,na kiutendaji.

Ukweli wa ushauri na wazo langu mtanzania mnyonge na nisie na elimu upo wazi kwa wenye weredi wa uzalendo,uadirifu,uchungu na maono ya kulivusha taifa kwenda kwenye raha,furaha na vicheko vya mafanikio.

Tafiti za kifisadi na za kuwafurahisha wafadhili wa nje ya nchi,mabosi na watupa misaada ya kondom,vyandarua,na elimu ya kujaamiana nadhani hazina nafasi ktk Tanzania mpya inayojengwa sasa.Tunahitaji tafiti za kutufanya tuwe wawekezaji ktk viwanda,mashamba,migodi,ufugaji,uvuvi,n.k.
 
========
hujatoa hoja ya msingi... unatakiwa ueleze jambo likamilike lieleweke. Kama unasema kuna upungufu wa bidhaa kupitia bandalini ushahidi uko wapi? kama kunaupungufu unatuhakikishiaje kwamba ni kwasababu ya mfumo na co kwamba kunasababu nyingine.... sio kila ugonjwa ni malaria eti kisa mgonjwa anatapia... So jenga hoja ndugu...
 
Asante kwa ushauri mwanajamvi,Mitandao ya kijamii ni platform rasmi katika utoaji taarifa,usambazaji taarifa na uelimishaji jamii,umma na wadau...Ingekuwa vema sana kama wahusika wakuu kiusimamizi na kiutendaji wangejitokeza wazi na kukana au kukubali taarifa au tetesi husika..Ukimya una maana kubwa sana ukiweza kutafakari kwa hekima ndogo au busara kiduchu kidunia..
Yapo baadhi yameanza kufanyiwa kazi na wahusika kikwazo kikubwa kikiwa ni ushirikiano mbovu wa kitaasisi {kisiasa/kiusimamizi/kiutekelezaji}..Maamuzi ya kisiasa ndio yenye nguvu katika zama tulizopo ..kilio changu mtanzania mnyonge ni kwa niaba ya wanyonge wengine haijarishi nafaidika kwa namna moja au nyingine au lah...

Lets constructively support our dear country to grow prosperously kupitia hata ushauri mdogo tunaoutoa credibly honestly..majungu,vijembe,nongwa,kejeli,dharau, Kiburi cha ufahamu,n.k ndivyo vilivyotufikisha tulipo..Inatosha..
 
MFUMO WA PAMOJA WA FORODHA{SINGLE CUSTOMS TERRITORY} UNASABABISHA MADHARA MAKUBWA HASA YA KIMAPATO KWA BANDARI ZETU HIVYO KUDIDIMIZA JITIHADA ZA NCHI KUJITEGEMEA KATIKA KUSUKUMA KASI YA MAENDELEO KWA KUTUMIA MAPATO YA NDANI.

Nianze kwa kupongeza juhudi za dhati za serikali ya awamu ya tano kufanya utakaso wa uozo mwingi ktk bandari kuu Tanzania.Nipongeze kwa dhati umakini mkubwa wa Waziri Mkuu Mh.Majaliwa na wote wanaompa taarifa nyeti kwa maslahi ya taifa.

Mizigo inayopita katika bandari zetu imepungua sana sana japo takwimu zaweza kufichwa lakini ukweli upo wazi..hivyo mapato yamepungua mno,athari kwa wadau ni kubwa mno,athari kwa sekta ya wawakirishi wa wenye meli...Pamoja na mdororo mdebwedo wa uchumi wa dunia lakini pia mfumo wa SCT ni moja ya sababu.

Tunaihitaji sana nchi ya Congo DR{Serikali,Wafanyabiashara-wadogo kwa wakubwa,wapya kwa wazamani} katika kufanikisha malengo yetu kimapato na kibiashara kwa maslahi ya taifa.

Lazima tukubali kwamba Kuhihusisha Congo DRC ktk mfumo wa utoaji/usafirishaji nje mizigo kupitia bandari za nchi wanachama wa Jumuiya ya Africa Mashariki kuna athari kubwa sana kwa uchumi wa nchi yetu {Tanzania}..Wateja wengi wamekimbia kutumia kutumia bandari zetu ..na ikumbukwe Importers and exporters toka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo wamekuwa wakibeba asilimia kubwa sana ya waagizaji wa nchi jirani wanaopitishia mizigo katika bandari za Tanzania na hata Mombasa {Kenya}.

Zaidi sana hata mizigo mingi iliokuwa inaagizwa na waagizaji wa Nchi za Rwanda na Burundi watumiaji wa mwisho wa bidhaa husika walikuwa ama ni wakongo toka maeneo yanayopakana na nchi husika.

Nini Ubaya wa Single Customs Territory na mfumo wake?

Mfumo unawalazimu waagizaji kuwa na mtaji mkubwa sana kibiashara unaoweza kufanikisha malipo ya ununuzi wa mzigo,usafiri,kodi na gharama zingine huku wakisubiri kwa muda mrefu pasipo mizigo husika kuwafikia.Hili limewafanya wafanyabiashara kubeba mzigo mkubwa hata kufanya biashara husika kuwa kama adhabu,mateso,shida hasa wanapotumia milango bahari ktk nchi zenye mfumo tajwa.

Mfumo unawalazimisha waagizaji toka nchi wanachama wa EAC na nchi waalikwa {Congo DRC} kulipa ushuru na kodi zote kabla mizigo haijatolewa katika bandari hususani ya Dar es salaam hivyo kubeba risks kubwa kibiashara kutokana na udhaifu wa mifumo na miundombinu hasa katika usafirishaji kupitia barabara,wizi,uharibifu.

Ucheweleshaji wa kutoa mizigo unaotokana na mwingiliano wa uhakiki,ufuatiliaji,tathmini,ukaguzi baina ya taasisi au mamlaka za kodi katika nchi ambazo mzigo unapitia/fikia/kombolewa kiforodha.Ucheweleshaji husika hupelekea gharama kuongezeka maradufu hasa ukihusisha tozo za ziada ktk bandari {port charges-removal,storage charges},mamlaka za kodi {Customs warehousing rent} na wamiriki makasha {demmurage charges} kwa mizigo iliohifadhiwa makashani {containerised cargoes}.

Ukosefu wa ushirikiano wa dhati baina ya wadau wa bandari kuu hivyo kupelekea mikwamo ya maamuzi ktk utekeleaji mkakati kwa maslahi ya taifa.Mfano ni uwepo wa wamiriki wa bandari kavu wenye maono ya kupata faida tu wakati wote,popote,vyovyote hapa katika mazingira ambayo wanapaswa kupata hasara kidogo kwa ajili ya mkakati wa makusudi kupata faida kubwa mbeleni.Vivo hivyo ushirikiano baina ya mamlaka za bandari,TRA na mawakala wa forodha..Kumekuwepo na uadui mkubwa na kuwindana badara ya ushirika mtakatifu kwa maslahi ya taifa.Mfano. Bandari wanapomchaji mteja storage charge hapo hapo TRA wanamchaji mteja huyo huyo Customs warehousing rent {equivalent to storage charge though they differ in calculations formula}.

Mapendekezo:
-Serikali ichukue hatua mahsusi za kidiplomasia kwa kupitia upya makubaliano yaliofikiwa kupitia EAC.

-Serikali ifanye tathmini ya kina ya madhara tajwa kwa kupitia ripoti zilizopo TRA/TPA na ikithibitika hasara tajwa isitishe kwa dhalura ushiriki wa nchi ya Congo DR ktk mfumo wa SCT.

-Walioshiriki kupendekeza mapendekezo yenye mapungufu kwa nchi yetu waangaliwe kwa jicho la nne ili iwe fundisho kwa wengine wanaofanya maamuzi yanayoigharimu nchi na vizazi vilivyopo na vijavyo.

-TPA kupitia ofisi yao ya Lubumbashi-Democratic Republic of Congo wawezeshwe kimkakati ili kuwashawishi wateja wengi waliokimbilia katika bandari za nchi jirani zisizo na mfumo wa SCT kama Namibia-Welvis Bay Port,Msumbiji-Beira Port,Afrika Kusini-Durban port na Angola-Lobito Port.

-Serikali ifanye maamuzi ya kuipatia serikali ya Kongo eneo mahsusi kuwa Bandari kavu kwa ajili ya kusaidia kushusha tozo adhabu{ kwa mizigo inayokwenda Kongo} zinazofanya bandari yetu kuwa ghali kibiashara hivyo kudidimiza ustawi kibiashara {vital essence in international trade/Supply chain/International Logistics }.

-Kitengo cha Huduma kwa wateja wa bandari zetu kiimalishwe na kifanye kazi kwa weredi uzalendo na kwa maslahi mapana ya nchi {Great Care and Attention} kwa kuhakikisha wadau wote wa bandari wanatoa huduma za kisasa,ubora,kwa unafuu na kwa haraka sana na si kama ilivyo sasa ambapo Rushwa,wizi,utapeli,uongo,ucheweleshaji,ufinyu wa utoaji taarifa,usumbufu n.k vimekuwa vitu vya kawaida wanavyotuhumiwa navyo sana wafanyakazi wa TPA,TRA,ICD's,Mawakala wa Forodha {CFA}.

-Kutengenezwe Transit informations centres maalumu kwa ajili ya kuwahudumia wateja wa nchi jirani zikiwa na huduma muhimu kuvutia wateja zaidi kurudi tena na tena {kama taarifa za bandari,mawakala,utalii,malazi,barabara,shopping,starehe etc}
Weka hapa takwimu za kushuka kwa mapato ya bandari! Wezi wakibanwa hupiga kelele...
 
Dah we utakuwa mzalendo sana, hongera sana kwa uchambuzi makini , big up, nadhani mawazo yako yote yakifanyiwa kazi basi mizigo na mapato yataongezeka
mwambie aweke vielelezo au takwimu wa kushuka mapato hapo ndipo utajua alivyo mzalendo.
 
Back
Top Bottom