Waziri Mkuu Majaliwa(CCM) ni Master wa time Management-Big Up!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Kama kuna jambo lililonivutiwa kuhusu utendaji wa Waziri Mkuu wetu Majaliwa (CCM) jinsi anavyoutumia muda wake kwa umakini na ufanisi mkubwa!

Nitatoa mifano miwili ambayo ndiyo imenisukuma kusema hivi kwa mfano alialikwa Moshi kwenye Sherehe za kusimikwa Askofu wa KKKT alivyokuwa huko akafanya safari ya kushtukiza Hospitali Kuu ya Mkoa Mawenzi ambapo haikuwa kwenye ratiba hivi juzi alihudhuria mazishi ya Baba yake (Apumzike kwa Amani) Waziri wetu wa Afya Waziri Mwalimu (CCM) huko Tanga hapo hapo akachepuka kutembelea Bandari ya Tanga na huko kuibua madudu!

Sina uhakika kama ndivyo walivyopanga kufanya kazi au ni ubunifu wake yeye Waziri Mkuu lkn vyovyote vile ni jambo zuri sana kwani linasevu fedha hapo ameua ndege wawili kwa jiwe moja!

Hongera Waziri Mkuu Majaliwa kwa huwo Ubunifu wa kutumia vizuri na kulinda rasimali fedha zetu ambazo tunazihitaji sana kwenye mambo mengine ya kimaendeleo tuko pamoja!

HAPA KAZI TU!
 
Hivi ziara ya kushtukiza unawaalika na wapiga picha/waandishi wa habari wa TV na magazeti? TAFAKARI...Mkwere alianzaga hivi hivi mara ziara za kila wizara ghafla ziara za masokoni (Tandika na Tandale) yaliyotokea tunayajua
 
Hongera ya nini ni sawa na baba kuwa nyumbani aamue kwenda jikoni kuangalia ela ya chakula ya mwezi anayompa mkewe vitu vya jumla anatekeleza au ameitumia kwa matumizi mengine sasa hadi uwajibu wa mtu katika kazi tunasifiana
 
Kwani kutoa hongera siyo haki yangu ya kikatiba kama MtanZania?
 
wanasema kua anatafuta sifa, ila mimi mwenyewe nampongeza maana tungeweza kupata ambaye hata hafuatilii chochote ili kupata hizo sifa na still akaendelea kua waziri mkuu,
vp kuhusu ile ishu ya kupewa maelezo na jamaa wa bandari ya tanga mwisho saa sita mchana wa leo, maana imeshapita muda imekuaje??
 
Huyu jamaa kafanana kwa Mbali na yule Dr. Sheen (PhD) toka Zanzibar (Hair style)
 
wanasema kua anatafuta sifa, ila mimi mwenyewe nampongeza maana tungeweza kupata ambaye hata hafuatilii chochote ili kupata hizo sifa na still akaendelea kua waziri mkuu,
vp kuhusu ile ishu ya kupewa maelezo na jamaa wa bandari ya tanga mwisho saa sita mchana wa leo, maana imeshapita muda imekuaje??

Nilichomaanisha ni hiyo time management yake yaani kuunganisha matukio ili kuokoa muda na fedha zetu kwa maana kama hii safari ya Tanga Bandarini ilibidi ni lazima aje siku moja na hii msiba pia ni lazima aende sasa ile kuamua kwamba kwa kuwa nipo Tanga kimsiba kwa nini pia basi nisilimalize na hili la kwenda Bandarini?
Wakati angekuwa Kiongozi mwingine angegawanya muda kwenye msiba na kwenda Bandarini kuwa siku mbili tofauti kama vile alivyofanya Moshi pia ndicho nilichomaanisha!
 
r
Hongera Magufuli kwa kutupa WAZIRI MKUU makini ambaye watanzania hatukutarajia kumpata. He is a very smart guy.
 
Hivi ziara ya kushtukiza unawaalika na wapiga picha/waandishi wa habari wa TV na magazeti? TAFAKARI...Mkwere alianzaga hivi hivi mara ziara za kila wizara ghafla ziara za masokoni (Tandika na Tandale) yaliyotokea tunayajua
Waandishi walikuwa kwenye msafara wa kwenda msibani, ghafla Mh Majaliwa akaesama pinda kushoto convoy yote lazima ifuate, including waandishi, ndo akaibukia bandarini...
 
Kitu kimoja wapaswa kujua,Rais,Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wana timu ya waandishi wa habari na waandishi hao ni sehemu ya misafara yao hivyo wanareport chochote kinachofanywa na viongozi hawa kama wakitakiwa kufanya hivyo..!
 
Nilichomaanisha ni hiyo time management yake yaani kuunganisha matukio ili kuokoa muda na fedha zetu kwa maana kama hii safari ya Tanga Bandarini ilibidi ni lazima aje siku moja na hii msiba pia ni lazima aende sasa ile kuamua kwamba kwa kuwa nipo Tanga kimsiba kwa nini pia basi nisilimalize na hili la kwenda Bandarini?
Wakati angekuwa Kiongozi mwingine angegawanya muda kwenye msiba na kwenda Bandarini kuwa siku mbili tofauti kama vile alivyofanya Moshi pia ndicho nilichomaanisha!
nafahamu ulichomaanisha ndioa maana nimempongeza, sasa naomba unipe mrejesho imekuaje kama unajua
 
Hivi ziara ya kushtukiza unawaalika na wapiga picha/waandishi wa habari wa TV na magazeti? TAFAKARI...Mkwere alianzaga hivi hivi mara ziara za kila wizara ghafla ziara za masokoni (Tandika na Tandale) yaliyotokea tunayajua
Tatizo lako ni uelewa, ila naamini iko siku utakuwa mwelewa, ila tu punguza mambo ya kukarrishwa, hivi ww unafikiri waziri mkuu ni mtu wa kawaida sana kwa akili yako, hata akina Mbowe bado wandishi wa habari wanawafuatilia kwa ukaribu sana ili upewe habari, kwa vyovyote vile huwezi kumtenganusha waziri mkuu na vyombo vya hbr bila hata kuvialika.
 
Hivi ziara ya kushtukiza unawaalika na wapiga picha/waandishi wa habari wa TV na magazeti? TAFAKARI...Mkwere alianzaga hivi hivi mara ziara za kila wizara ghafla ziara za masokoni (Tandika na Tandale) yaliyotokea tunayajua

Kama hujui waziri mkuu anatembea na waandishi wa habari bas kaa kimyaa
 
Waandishi walikuwa kwenye msafara wa kwenda msibani, ghafla Mh Majaliwa akaesama pinda kushoto convoy yote lazima ifuate, including waandishi, ndo akaibukia bandarini...
Are u Sure..?
uliza waliokuwepo, sio kuandika tu.
 
Kama kuna jambo lililonivutiwa kuhusu utendaji wa Waziri Mkuu wetu Majaliwa (CCM) jinsi anavyoutumia muda wake kwa umakini na ufanisi mkubwa!

Nitatoa mifano miwili ambayo ndiyo imenisukuma kusema hivi kwa mfano alialikwa Moshi kwenye Sherehe za kusimikwa Askofu wa KKKT alivyokuwa huko akafanya safari ya kushtukiza Hospitali Kuu ya Mkoa Mawenzi ambapo haikuwa kwenye ratiba hivi juzi alihudhuria mazishi ya Baba yake (Apumzike kwa Amani) Waziri wetu wa Afya Waziri Mwalimu (CCM) huko Tanga hapo hapo akachepuka kutembelea Bandari ya Tanga na huko kuibua madudu!

Sina uhakika kama ndivyo walivyopanga kufanya kazi au ni ubunifu wake yeye Waziri Mkuu lkn vyovyote vile ni jambo zuri sana kwani linasevu fedha hapo ameua ndege wawili kwa jiwe moja!

Hongera Waziri Mkuu Majaliwa kwa huwo Ubunifu wa kutumia vizuri na kulinda rasimali fedha zetu ambazo tunazihitaji sana kwenye mambo mengine ya kimaendeleo tuko pamoja!

HAPA KAZI TU!
Tunataka wabadili mfumo sio hz ishu za kustukiza hazina tija kwa taifa.
Walete dawa ya majipu kuibuka kila mahala, sio kutumbua na kuondoka.
 
Back
Top Bottom