Waziri Mkuu kutumbua majipu Kanda ya Ziwa yaliyomshinda Nyerere?

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,575
Majaliwa au ‘Mzee wa Bandari’, anavyoitwa siku hizi, anazuru mikoa ya Kanda ya Ziwa, ambako hakuna shaka amekutana na kero lukuki, baadhi yake zikiwa zimedumu kwa miaka takriban 55 ya uhuru wa nchi yetu, ingawa zipo mpya.

Miongoni mwa kero za wananchi, hasa kwa upande wa kanda hiyo yenye utajiri mwingi ni pamoja na mwingiliano mkubwa wa wageni uliosababisha
uhalifu na kuzagaa kwa silaha.

Kuhusu hili la wageni kuingia nchi hii yenye ukarimu mwingi, bila shaka Mzee wa Bandari atakuwa amekutana nalo kwenye mikoa yote, ingawa Kagera na Geita litakuwa kubwa zaidi.

Namuomba mzee huyu asishangae, akiwa Kagera tangu juzi atambue tatizo hili lipo kwa siku nyingi, tangu zama za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Yeye (Mwalimu Nyerere), alikemea utumikishaji wa watu (Warundi), kwenye mashamba ya migomba na kahawa, ambako kwa wenyeji ni jambo la kawaida,ingawa kwa siku za karibuni, Idara ya Uhamiaji, eti, imeshtuka na kuanza kuwachukulia hatua.

Ni nani asiyejua jinsi Warundi walivyogeuzwa wapagazi kwenye mashamba kule Karagwe, Muleba, Missenyi, Bukoba mkoani Kagera, tena kwa miaka mingi?

Niseme wazi, Mwalimu Nyerere wakati wa ziara zake mkoani Ziwa Magharibi,sasa Kagera aliwaonya wakazi wake kuacha tabia za kuwatumikisha na kuwamiliki binadamu wenzao, huku wakitamka, ‘ninaye Mrundi wangu’.

Ukiacha hili la Warundi, tunaoelezwa sasa na Uhamiaji kuwa ni wahamiaji haramu, wamekuwa vibarua kwenye mashamba, naamini hata gavana wa mkoa huo, John Vianney Mongella atakuwa tayari amemweleza bosi wake, Waziri Mkuu Majaliwa aliyoyaona kwenye mapori ya Karagwe ambako alikutana na wakimbizi wakidai ni Watanzania, lakini hawajui jiografia ya nchi hii.

Hao wameajiriwa na wakazi wa mkoa huo kwa kazi za kuchunga ng’ombe au wao na wazazi wao wanaishi kwenye mapori na ng’ombe wao.

Matokeo ya umiliki huo haramu wa ardhi, baadhi yao wamekua, wameoa na sasa si Watanzania wala Wanyarwanda, ila wanaishi Tanzania, wako Karagwe, Muleba na Ngara, pori la Kimisi limejaa, wanamiliki makundi makubwa ya ng’ombe, wanaonekana wavamizi.

Mbali ya hao, wapo wakimbizi wa Kinyarwanda wa miaka mingi iliyopita na wengine wapya, mwaka 1994, waliingia Tanzania na makundi makubwa ya
ng’ombe, aina ya Ankole, wamegeuka wenyeji, kiasi kwamba wazawa waliojaribu kufuga hawana chao, wanakosa mahali pa kuchungia mifugo yao.

Kitu kingine ninachoamini viongozi wa mkoa wa Kagera, labda kama gavana Mongella aliambiwa, kisha naye amemweleza mgeni wake, Waziri Mkuu, ni
baadhi ya viongozi wa vijiji, kata, tarafa na wilaya kutumia ujio huo wa wafugaji wa Kinyarwanda kuchuma mali, kwa maana ya ng’ombe, ambao huwachukua kutoka kwa wafugaji kama zawadi na wakati mwingine rushwa.

Si viongozi peke yao, bali hata walinda amani, yaani polisi na hata mahakimu, baadhi yao wametajirika kwa miaka mingi, wameishi kwa rushwa
kutoka kwa wafugaji wenye asili ya Rwanda, kiasi kwamba haki hauitendeki. Ni rushwa hiyo hiyo imehamia kwenye ubinafsishaji wa mashamba ya mifugo ya Serikali, yaani ranchi ile ya Kitengule, Mabale,Kagoma na nyingine, ambako wafugaji wazawa wametupwa nje, kumekuwa na upendeleo, wageni au wawekezaji wamebebwa, kiasi cha wazawa kunyanyaswa.

Ni ajabu, lakini lazima Waziri Mkuu Majaliwa atumbue jipu hili lililowashinda viongozi wengi, watangulizi wake waliofika au kuishi Kagera.

Ipo migogoro baina ya wafugaji wa kata mbalimbali za wilaya ya Karagwe,zinazopakana na ranchi ya Kitengule na nyinginezo, wafugaji wazawa wao
ndio wakimbizi kwani ng’ombe mmoja akivuka na kuingia kwenye maeneo yanayomilikiwa na wawekezaji, basi faini ni Sh20,000 au zaidi, jambo linalowafilisi.

Faini hizo za ovyo zimegeuka sehemu ya maisha Karagwe, Muleba, kidogo Ngara, Biharamulo, ingawa haziingii kwenye mfuko wa serikali ya wilaya
hizo na kama viongozi wanabisha, wajitokeze hadharani wamweleze Waziri Mkuu Majaliwa kiasi cha fedha walizo nazo kutokana na faini na
kimekusanywa kwa miaka mingapi.

Ni vyema Waziri Mkuu Majaliwa akiwa Kagera, kwa mfano awatake ma-DC,Deodatus Kinawiro (wa Karagwe na wenzake wa Muleba, Isaack Francis au Darry Regasira wa Biharamulo na wasaidizi wao wamweleze jinsi gani walivyosaidia kutatua migogoro ya wafugaji kwenye maeneo yao.

Kwa Karagwe, zipo kata za Kihanga, Igurwa, Kanoni, Ruhita na nyinginezo nyingi, ambazo watu wake wamenyanyaswa kwa miaka mingi, ng’ombe na
mifugo yao mingi imezuiwa kwa madai ya kuingilia maeneo ya wawekezaji.

Mwishowe, Majaliwa, inafaa uangalie pia ushirika, mkombozi wa wakulima wa Kagera kwa miaka mingi ambao pamoja na vyama vyake vya kuweka na
kukopa umejifia.

Ushirika umetafunwa na wajanja, Majaliwa waombe viongozi wako wakuambie wanafanya nini ili kuufufua ili wakulima waishi vizuri kama ilivyokuwa zamani.
 
ahahahahahahahahahahahhaah

Niwaulize kwani tangu ameenda bandari...what has changed so far?
 
hawatumbue tu kwani warundi na wanyarwanda wanatuharibia ruga ya kihaya kwa kuchanganya kiruga chao, pia kutupigia wake zetu na kuzaa mbegu za watu wenye hasira sana kutokana na mienendo yao na tabia zao za kivita vita, watoto wanazaliwa na hasira mbaya. kwa kweli wakina kyataye minane ni shida hasa wilaya ya karagwe, biharamulo na muleba kusini
 
kihelele chako; unadanganywa na sura ya kinyarwanda ; Unaoa kumbe madhara ni kizazi chako , kinakuwa cha hasira,
Dadazako hawapo mpk kuoa wanyarwanda?????????????????????
 
Majaliwa au ‘Mzee wa Bandari’, anavyoitwa siku hizi, anazuru mikoa ya
Kanda ya Ziwa, ambako hakuna shaka amekutana na kero lukuki, baadhi yake
zikiwa zimedumu kwa miaka takriban 55 ya uhuru wa nchi yetu, ingawa zipo
mpya.

Miongoni mwa kero za wananchi, hasa kwa upande wa kanda hiyo yenye
utajiri mwingi ni pamoja na mwingiliano mkubwa wa wageni uliosababisha
uhalifu na kuzagaa kwa silaha.

Kuhusu hili la wageni kuingia nchi hii yenye ukarimu mwingi, bila shaka
Mzee wa Bandari atakuwa amekutana nalo kwenye mikoa yote, ingawa Kagera
na Geita litakuwa kubwa zaidi.

Namuomba mzee huyu asishangae, akiwa Kagera tangu juzi atambue tatizo
hili lipo kwa siku nyingi, tangu zama za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius
Nyerere.

Yeye (Mwalimu Nyerere), alikemea utumikishaji wa watu (Warundi), kwenye
mashamba ya migomba na kahawa, ambako kwa wenyeji ni jambo la kawaida,
ingawa kwa siku za karibuni, Idara ya Uhamiaji, eti, imeshtuka na kuanza
kuwachukulia hatua.

Ni nani asiyejua jinsi Warundi walivyogeuzwa wapagazi kwenye mashamba
kule Karagwe, Muleba, Missenyi, Bukoba mkoani Kagera, tena kwa miaka mingi?

Niseme wazi, Mwalimu Nyerere wakati wa ziara zake mkoani Ziwa Magharibi,
sasa Kagera aliwaonya wakazi wake kuacha tabia za kuwatumikisha na
kuwamiliki binadamu wenzao, huku wakitamka, ‘ninaye Mrundi wangu’.
Ukiacha hili la Warundi, tunaoelezwa sasa na Uhamiaji kuwa ni wahamiaji
haramu, wamekuwa vibarua kwenye mashamba, naamini hata gavana wa mkoa
huo, John Vianney Mongella atakuwa tayari amemweleza bosi wake, Waziri
Mkuu Majaliwa aliyoyaona kwenye mapori ya Karagwe ambako alikutana na
wakimbizi wakidai ni Watanzania, lakini hawajui jiografia ya nchi hii.

Hao wameajiriwa na wakazi wa mkoa huo kwa kazi za kuchunga ng’ombe au
wao na wazazi wao wanaishi kwenye mapori na ng’ombe wao.

Matokeo ya umiliki huo haramu wa ardhi, baadhi yao wamekua, wameoa na
sasa si Watanzania wala Wanyarwanda, ila wanaishi Tanzania, wako
Karagwe, Muleba na Ngara, pori la Kimisi limejaa, wanamiliki makundi
makubwa ya ng’ombe, wanaonekana wavamizi.

Mbali ya hao, wapo wakimbizi wa Kinyarwanda wa miaka mingi iliyopita na
wengine wapya, mwaka 1994, waliingia Tanzania na makundi makubwa ya
ng’ombe, aina ya Ankole, wamegeuka wenyeji, kiasi kwamba wazawa
waliojaribu kufuga hawana chao, wanakosa mahali pa kuchungia mifugo yao.

Kitu kingine ninachoamini viongozi wa mkoa wa Kagera, labda kama gavana
Mongella aliambiwa, kisha naye amemweleza mgeni wake, Waziri Mkuu, ni
baadhi ya viongozi wa vijiji, kata, tarafa na wilaya kutumia ujio huo wa
wafugaji wa Kinyarwanda kuchuma mali, kwa maana ya ng’ombe, ambao
huwachukua kutoka kwa wafugaji kama zawadi na wakati mwingine rushwa.

Si viongozi peke yao, bali hata walinda amani, yaani polisi na hata
mahakimu, baadhi yao wametajirika kwa miaka mingi, wameishi kwa rushwa
kutoka kwa wafugaji wenye asili ya Rwanda, kiasi kwamba haki
hauitendeki. Ni rushwa hiyo hiyo imehamia kwenye ubinafsishaji wa
mashamba ya mifugo ya Serikali, yaani ranchi ile ya Kitengule, Mabale,
Kagoma na nyingine, ambako wafugaji wazawa wametupwa nje, kumekuwa na
upendeleo, wageni au wawekezaji wamebebwa, kiasi cha wazawa kunyanyaswa.

Ni ajabu, lakini lazima Waziri Mkuu Majaliwa atumbue jipu hili
lililowashinda viongozi wengi, watangulizi wake waliofika au kuishi Kagera.

Ipo migogoro baina ya wafugaji wa kata mbalimbali za wilaya ya Karagwe,
zinazopakana na ranchi ya Kitengule na nyinginezo, wafugaji wazawa wao
ndio wakimbizi kwani ng’ombe mmoja akivuka na kuingia kwenye maeneo
yanayomilikiwa na wawekezaji, basi faini ni Sh20,000 au zaidi, jambo
linalowafilisi.

Faini hizo za ovyo zimegeuka sehemu ya maisha Karagwe, Muleba, kidogo
Ngara, Biharamulo, ingawa haziingii kwenye mfuko wa serikali ya wilaya
hizo na kama viongozi wanabisha, wajitokeze hadharani wamweleze Waziri
Mkuu Majaliwa kiasi cha fedha walizo nazo kutokana na faini na
kimekusanywa kwa miaka mingapi.

Ni vyema Waziri Mkuu Majaliwa akiwa Kagera, kwa mfano awatake ma-DC,
Deodatus Kinawiro (wa Karagwe na wenzake wa Muleba, Isaack Francis au
Darry Regasira wa Biharamulo na wasaidizi wao wamweleze jinsi gani
walivyosaidia kutatua migogoro ya wafugaji kwenye maeneo yao.

Kwa Karagwe, zipo kata za Kihanga, Igurwa, Kanoni, Ruhita na nyinginezo
nyingi, ambazo watu wake wamenyanyaswa kwa miaka mingi, ng’ombe na
mifugo yao mingi imezuiwa kwa madai ya kuingilia maeneo ya wawekezaji.

Mwishowe, Majaliwa, inafaa uangalie pia ushirika, mkombozi wa wakulima
wa Kagera kwa miaka mingi ambao pamoja na vyama vyake vya kuweka na
kukopa umejifia.

Ushirika umetafunwa na wajanja, Majaliwa waombe viongozi wako wakuambie
wanafanya nini ili kuufufua ili wakulima waishi vizuri kama ilivyokuwa
zamani.

Habari ndeefu lkn umeandika upupu mtupu!
 
Hii thread yako ni ya kanda ya ziwa au ya mkoa wa Kagera?
 
Nategemea tunayo yaona Kagera,Kigoma,huwezi kuyaona Ruvuma,Mtwara,Arusha, nikimaanisha Mikoa yote imepakana na majirani zetu,ila naona maongezi na mijadara mingi na muingiliano hupo katika mikoa miwili,
Kwanini siyo Jaruo ,Masai,Mngoni,Mmeru nk, Ila Murundi na Mnyarwanda ndo sumu.
Tunaomba mtujuze wadadavuzi
 
Back
Top Bottom