Waziri Mkuu: Kampuni za watumishi zisipewe zabuni ndani ya Halmashauri wanazozitumikia


Mondoros

Mondoros

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2015
Messages
631
Likes
410
Points
80
Mondoros

Mondoros

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2015
631 410 80
pol-jpg.443168


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Bi. Theresia Mahongo kuhakikisha kampuni zinazomilikiwa na madiwani na watumishi wa halmashauri hiyo hazipewi zabuni zinazotolewa katika maeneo yao kwa ajiliya kuepusha migongano ya kimaslahi.

Ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Desemba 5, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Karatu mkoani Arusha katika ukumbi bwalo la Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Karatu akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani hapa.

"Hauzuiliwi kufanya biashara ili mradi kampuni yako isifanye kazi katika halmashauri ambayo wewe unaitumikia na una nguvu nayo ili kuepusha migongano ya kimaslahi kwani miradi yote utajilundikia," amesema.
Pia amewataka Wakuu wa Idara katika halmashauri hiyo walisaidie Baraza la Madiwani katika kubaini vyanzo vipya vya mapato kwa lengo la kuongeza mapato ya halmashauri yao.

Wakati huo huo Waziri Mkuu amewataka watumishi wa halmashauri wa umma kujitathmini na kujiridhisha kama wanafuata misingi ya utumishi katika utendaji kazi wao wa kila siku. Amewasisitiza wawatumikie wananchi kwa uadilifu na uaminifu mkubwa.

"Hatuhitaji kuwa na mtumishi mvivu, asiyewajibika, mwizi, mla rushwa na asiyekuwa muadilifu mahali pa kazi.Na atakayeona ameshindwa kutunza na kusimamia fedha za miradi ya maendeleo ya wananchi atoe taarifa hatutaki watu kufanya kazi kwa mazoea," amesema.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa " watumishi wa umma lazima mbadilike na muwe na nidhamu ya kazi. Muache malalamiko fanyeni kazi na msitafute sympathy (huruma) kutoka kwa watu kwani Serikali haitamuonea mtumishi yeyote ," amesema.

Amesema katika baadhi ya ofisi za Serikali kuna ugonjwa wa watumishi wanapoona wageni wamelifika kwa ajili ya kupatiwa huduma wanawapita bila ya kuwasikiliza. " sasa hatutaki watumishi wa namna hiyo, Jukumu lako ni kumtumikia Mtanzania na tunataka kuona mabadiliko. Hatutaki kuona watu wakizubaa maofisini,".

Waziri Mkuu amesema Serikali ikikuta wananchi wanalalamika kutokana na kutoridhishwa na huduma zitolewazo na watumishi wa umma itahakikisha watumishi hao wanachukuliwa hatua. Serikali ni ya Watanzania wote hivyo lazima wahudumiwe vizuri bila ya kujali uwezo wao kifedha wala itikadi zao za kidini na kisiasa.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMATATU, DESEMBA 5, 2016.
 
N

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Messages
23,791
Likes
27,956
Points
280
N

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined Aug 1, 2007
23,791 27,956 280
Yuko sahihi
 
No Escape

No Escape

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2016
Messages
5,323
Likes
5,402
Points
280
No Escape

No Escape

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2016
5,323 5,402 280
Ahsante! Kama ni kweli,hapa amewapatia...
 
Ndalama

Ndalama

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2011
Messages
8,531
Likes
5,485
Points
280
Ndalama

Ndalama

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2011
8,531 5,485 280
Kwani ni kauli mpya?
 
Ekyoma

Ekyoma

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Messages
1,905
Likes
2,369
Points
280
Ekyoma

Ekyoma

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2015
1,905 2,369 280
Wazir mkuu anafaa zaid kuliko bwana yule
 
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2015
Messages
24,262
Likes
55,155
Points
280
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2015
24,262 55,155 280
Hiyo sio kauli mpya, tunachotaka ni utekelezaji
 

Forum statistics

Threads 1,273,061
Members 490,262
Posts 30,469,872