Waziri Mkuu Johnson kutoa vipaumbele vyake

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,419
Reaction score
5,021
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson leo hii anatarajiwa kuelezea mipango yake, ya namna gani atatekeleza ahadi zake za kufanikisha kujiondoa katika Umoja wa Ulaya haraka na kupanua wigo wa huduma za afya nchi mwake.

Katika hafla ya kuanza msimu mpya wa bunge la Uingereza, Malkia Elizabeth atazisoma sheria ambazo serikali ingetaka bunge la Uingereza liliziridhie na atatilia mkazo vipaumbele vya Johnson baada ya ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa juma lililopita.

Pamoja na masuala kadhaa na Umoja wa Ulaya kupaswa kufikiwa ifikapo 2020, Johnsonpia anatakiwa kufanikisha taifa lake kujitenga na Umoja wa Ulaya Januari 31 mwaka ujao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…