Waziri Mkuu hili la uchaguzi wa Meya wa jiji la Dsm kweli halikugusi?

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,345
Kadili muda unavyoenda na jinsi waziri wa Tamisemi anavyoingilia kati kutaka kutatua mtanziko wa kumpata meya wa jiji la Dsm ndivyo anavyozidi kupuuzwa na mkurugenzi wa jiji hilo ambaye kiutendaji yuko chini yake. Inatia mashaka kwamba inawezekana kuna mkono wa kiongozi wa juu zaidi anayeukwamisha mambo kwa maslahi yake au ya chama chake.

Kama Rais siku zote tangu wakati wa uchaguzi alikuwa akiwaahidi watanzania kwamba atakuwa ni Rais wa watanzania wote, wa vyama vyote, makabila yote, dini zote na jinsia zote mbona sasa amekaa kimya wakati mambo ya kibaguzi yakifanywa jijini Dsm? Au haoni figisu figisu ya uchaguzi wa meya wa jiji la Dsm kama inayomgusa?
Au tuamini kwamba hilo linamhusu yeye binafsi kama Rais, lakini watendaji wake wakiendesha unyanyasaji na ubaguzi wa kivyama ktk jiji la Dsm halimhusu kwa sababu si yeye anayelisimamia?

Lakini Rais hana budi kukumbuka kwamba urais ni taasisi, kwa hiyo hana budi kuhakikisha kwamba serikali kwa niaba yake inafanya yale aliyowaahidi watanzania.
 
umehairishwa kwa miezi sita?
Madiwani wa ukawaa wajiandae kununuliwa nyumba masaki kila mmoja
 
Kimsingi hata raisi Magufuli yuko kibatili madarakani basi wanasheria wanapindisha sheria nakutuaminisha kura za bara na zanzibar nitofauti. Hakuna haja yakuwa namuungano tena huu ni unafiki uliokithiri.

Haiwezekani meya wa Dar wajumbe upande wa Ccm watoke Zanzibar ilihali uchaguzi wamefuta huku nikutufanya sisi wapigakura matahira.

Na pia kama wajumbe wanatoka Zanzibar basi uchaguzi wa raisi bara ni batili kabisa. Huu ni uhuni usio vumilika.
 
Back
Top Bottom