Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,559
- 1,180
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amewaelekeza wasimamizi wa uchaguzi katika mamlaka za serikali za Mitaa kuendelea kuhamasisha na kuweka mabango yanayoelekeza vituo vya kujiandikisha kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mhe. Katimba ametoa maelekezo hayo mkoani Kigoma kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa mara baada ya kujiandikisha katika kituo kilichopo katika shule ya msingi Kilimahewa kata ya Kilimahewa Manispaa ya Kigoma.
“Wasimamizi wa Uchaguzi wahakikishe kwamba vituo hivi vya uchaguzi vinajulikana kwa watanzania na watanzania waweze kufahamu ni maeneo gani na hivi vituo viko wapi hivyo wapitishe magari kwenye mitaa na vijiji kuwahamasisha watanzania waweze kujitokeza na wafahamu vituo vya kujiandikisha viko maeneo gani” amesema
Katika hatua nyingine Mhe. Katimba amefafanua kuwa zoezi hili lililoanza Oktoba 11,2024 na linatarajiwa kukamilika Oktoba 20,2024 ni kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27,2024 na zoezi hili halihusiani na uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura linaendelea katika kanda mbalimbali nchi ambalo ni kwaajili ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2025