Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba azindua Kituo Kikubwa Cha CNG Puma Energy

Blasio Kachuchu

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
573
Reaction score
359

Dar es Salaam, Februari 9, 2026

Kampuni ya Puma Energy Tanzania imezindua rasmi Kituo Mama cha Gesi Asilia Iliyoshindiliwa (CNG) kilicho kikubwa na cha kisasa zaidi barani Afrika, hatua inayotajwa kuwa ya kihistoria katika safari ya Tanzania kuelekea matumizi ya nishati safi, nafuu na rafiki kwa mazingira.

358495.jpg
Uzinduzi wa kituo hicho ulifanyika jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ambapo alieleza kuwa mradi huo ni uthibitisho wa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kukuza matumizi ya nishati mbadala na kuimarisha mazingira ya uwekezaji nchini.
Kituo hicho cha kisasa kimeundwa kukidhi ongezeko la mahitaji ya CNG kama mbadala wa mafuta ya petroli na dizeli, huku kikihudumia magari madogo, mabasi pamoja na malori makubwa. Aidha, kituo hicho kitafanya kazi kama kitovu kikuu cha usambazaji wa gesi kwenda vituo vingine vidogo vya CNG nchini kupitia trela maalum za kusafirisha gesi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Bi. Fatma Abdallah, alisema mradi huo unaakisi imani ya muda mrefu ya kampuni kwa Tanzania na dhamira yake ya kuchangia maendeleo endelevu ya Taifa.

“Kituo hiki Mama cha CNG ni zaidi ya miundombinu; ni ishara ya imani yetu kwa Tanzania na ushirikiano wetu na Serikali katika kuijenga nchi kupitia nishati safi na ya uhakika,” alisema Bi. Abdallah.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba alisema mradi huo ni mfano bora wa mafanikio ya ubia kati ya Serikali na sekta binafsi (PPP), akibainisha kuwa uwekezaji huo unachangia mapato ya Serikali, ajira na ujenzi wa miundombinu ya kimkakati.

358497.jpg
“Puma Energy Tanzania imeonesha mfano mzuri wa namna sekta binafsi inavyoweza kushirikiana na Serikali kuleta maendeleo yanayogusa maisha ya wananchi,” alisema Waziri Mkuu.
Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, alisema muundo wa umiliki wa Puma Energy Tanzania unaifanya Serikali kunufaika moja kwa moja na mafanikio ya kibiashara ya kampuni hiyo. Alisema ubia huo unaonesha kuwa kuchanganya ufanisi wa sekta binafsi na ushiriki wa Serikali kunazalisha manufaa makubwa kwa Taifa.

Katika kipindi cha ujenzi wa mradi huo, zaidi ya Watanzania 300 walipata ajira, wakiwemo wahandisi na mafundi zaidi ya 100, huku wakandarasi wa ndani na biashara ndogo na za kati (SMEs) wakipewa kipaumbele, hatua iliyochochea uchumi wa eneo husika.

Mkuu wa Idara ya Sheria na Mahusiano wa Puma Energy Tanzania, Wakili Emmanuel G. Bakilana, alisema uwekezaji huo ni sehemu ya dhamira ya muda mrefu ya kampuni nchini, akibainisha kuwa katika miaka mitatu iliyopita Puma Energy imelipa zaidi ya shilingi trilioni 1.4 kama kodi na ushuru, na mwaka 2025 ilitoa gawio la shilingi bilioni 21 kwa wanahisa.

Hafla ya uzinduzi ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Waziri wa Nishati, pamoja na wawakilishi wa taasisi za udhibiti kama EWURA, TPDC na TANESCO, hali iliyoonesha mshikamano na ushirikiano mkubwa katika kufanikisha hatua hiyo muhimu kwa sekta ya nishati nchini.
 
Attachments

  • Screenshot_20230930-090635_Samsung Internet.jpg
    Screenshot_20230930-090635_Samsung Internet.jpg
    190.1 KB · Views: 5
  • Screenshot_20230930-090531_Samsung Internet.jpg
    Screenshot_20230930-090531_Samsung Internet.jpg
    194.5 KB · Views: 4
  • Screenshot_20230930-090520_Samsung Internet.jpg
    Screenshot_20230930-090520_Samsung Internet.jpg
    200.1 KB · Views: 9
Hawana Pakwenda...Kazi Za Meya,,Wakurugenzi,,Wakuu Wa Wilaya,,Makatibu Tawala n.k
 
Back
Top Bottom