Waziri Mkuu ataka Ulinzi uimarishwe gereza la Lindi ambapo watuhumiwa wa dawa za kulevya wamefungwa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,880
6,367
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa amemtaka Mkuu wa Magereza mkoa wa Lindi, kuhakikisha hakuna mtuhumiwa wa dawa za kulevya atakayetoweka katika gereza la mkoa huo.

Amesema kuna watuhumiwa wa dawa za kulevya ambao wanahifadhiwa katika gereza la mkoa wa Lindi hivyo ni vema akajiridhisha kama ulinzi na usalama wa watuhumiwa hao umeimarishwa.

Hata hivyo, Waziri Mkuu Majaliwa amemtaka mkuu wa gereza hilo kuwa makini na baadhi ya zabuni wanazozitoa kutoka nje na kuhakikisha ulinzi unaimarisha wakati wote gerezani hapo.

Aidha Waziri Mkuu Majaliwa amemtaka mkuu huyo wa Magereza kujiridhisha kama ulinzi na usalama wao umeimarishwa na kuhakikisha hakuna mtuhumiwa anayetoweka.

Amesema matumizi ya dawa hizo yanasababisha kupunguza kwa nguvu kazi kwani watumiaji wengi ni vijana,hivyo alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na serikali katika kupiga vita matumizi ya dawa hizo kwa kuwafichua wauzaji na watumiaji.
 
Wakamatwe wote mkuu tunaungana nawe kwenye hilo hadi kieleweke.laiti huu uongozi ungeanza mwaka ya nyumba nchi ingekuwa imepiga hatua. I mean it really these drugs have eroded our bothers n' sisters MUNGU ubariki uongozi huu
 
Nahisi PM amenusa uwepo wa EL CHAPO wa aina yake katika gereza hilo ambaye anaweza kutoroshwa kama hawatachukuwa tahadhari mapema!
 
Watuhumiwa hawafungwi mkuu,wanawekwa rumande hivyo rekebisha kichwa cha habari kama hutajali
 
Justice delayed is justice denied. Hakuna sababu za msingi watuhumiwa wa madawa ya kulevya kuchukua muda mrefu kuhumiwa. Kama hawana hatia waachie la sivyo wafungwe. Hawa ni watu Mwenye ushawishi mkubws wa kifedha na wanaweza kutumia nguvu hiyo kughiribu lakini za Askari wa Magereza na kuweza kutoroka.
Hivyo hukumu ipitishwe mapema ili haki itendeke.
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa amemtaka Mkuu wa Magereza mkoa wa Lindi, kuhakikisha hakuna mtuhumiwa wa dawa za kulevya atakayetoweka katika gereza la mkoa huo.

Amesema kuna watuhumiwa wa dawa za kulevya ambao wanahifadhiwa katika gereza la mkoa wa Lindi hivyo ni vema akajiridhisha kama ulinzi na usalama wa watuhumiwa hao umeimarishwa.

Hata hivyo, Waziri Mkuu Majaliwa amemtaka mkuu wa gereza hilo kuwa makini na baadhi ya zabuni wanazozitoa kutoka nje na kuhakikisha ulinzi unaimarisha wakati wote gerezani hapo.

Aidha Waziri Mkuu Majaliwa amemtaka mkuu huyo wa Magereza kujiridhisha kama ulinzi na usalama wao umeimarishwa na kuhakikisha hakuna mtuhumiwa anayetoweka.

Amesema matumizi ya dawa hizo yanasababisha kupunguza kwa nguvu kazi kwani watumiaji wengi ni vijana,hivyo alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na serikali katika kupiga vita matumizi ya dawa hizo kwa kuwafichua wauzaji na watumiaji.
wanaoggopa yasije tokea ya EL Chapo..hahaha, safi
 
Nahisi PM amenusa uwepo wa EL CHAPO wa aina yake katika gereza hilo ambaye anaweza kutoroshwa kama hawatachukuwa tahadhari mapema!
Yawezekana kabisa kuwa kavujishiwa taarifa za baadhi ya watuhumiwa kuwa na mipango ya kutoroshwa!
 
Ni wazo zuri kuchukua tahadhari kwani huko nyuma enzi za Mwl,Nyerere (R.I.P) mtuhumiwa wa Uhaini Thomas Lugakingira au Father Tom au Uncle Tom, aliwahi kutoroka Gerezani kwa msaaada wa Askari Magereza hali hiyo ilipelekea aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini wakati huo Ndugu Gabriel Ganja Genea kujiuzuru.
 
PM anataka ulinzi uimarishwe wakati baadhi ya mahabusu wanashindwa kupelekwa mahakamani kwa magereza kukosa hela ya mafuta
 
Ni wazo zuri kuchukua tahadhari kwani huko nyuma enzi za Mwl,Nyerere (R.I.P) mtuhumiwa wa Uhaini Thomas Lugakingira au Father Tom au Uncle Tom, aliwahi kutoroka Gerezani kwa msaaada wa Askari Magereza hali hiyo ilipelekea aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini wakati huo Ndugu Gabriel Ganja Genea kujiuzuru.
Hata muuza madawa ya kulevya maarufu aliyewahi kufungwa ktk gereza mojawapo Dodoma aliyefahamika kwa jina LA akasha....alitoroka kwa kupewa msaada na askari magereza....
Tatizo askari magereza wengi wana hali ngumu kiuchumi kwa hiyo ikitokea wakioneshwa mlungula....ah watakutengenezea mchongo utoroke!
 
Back
Top Bottom