Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,876
- 2,747
Juzi hapa ndani ya Bunge la Jamhuri tulishuhudia Waziri Mkuu Mizengo Pinda akinasa kwenye mtego wa swali lililoulizwa na mh Wenje kuhusu madaraka na mamlaka ya watumishi wa umma kwa wananchi dhidi ya utumishi kwa chama kilichopo madarakani. Tulishuhudia Pinda akisema kuwa hao watumishi wa umma wakiwa ni pamoja na wakuu wa mikoa na wilaya wana haki ya kufanya kazi za chama ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa ccm kinaendelea kutawala...
Kabla yake, Rais alishawahi kutamka na kkuonya juu ya hao hao watumishi wa umma ambao walishasahau majukumu yao na kujiingiza kwenye siasa za ccm. Ndipo wakati wa kuteua wakuu wa wilaya na mikoa, Rais akawaonya na kuwaasa na kuwakaripia kuwa wasiende kufanya siasa bali kutumikia wananchi! Na yeyote atakayekwenda kinyume na hayo maagizo atatoswa! Sasa leo tena tunasikia eti wao ni ruksa kufanya kazi za chama ili kutekeleza ilani ya chama ikiwa ni pamoja na kuhakikisha ccm hakitoki madarakani.
Waziri Mkuu anapingana na Rais. Huu ni udhaifu wa taasisi ya urais au ni athari za uropokaji za PM, au ni mkakati wa ccm uliojificha ambao wenyewe wanaufichua bila kujua?