Kwa tukio hili tatizo si waziri mkuu ni spika, waziri mkuu alikuwa makini ndiyo maana hata baada ya kuulizwa mara tatu hakuteteleka nakumbuka mara ya mwisho alipoulizwa alisimama akasema 'NIMESEMA NDIO'. Imekuwa ni tendency ya wabunge wa CCM kupinga kila kinacholetwa na wapinzani, spika hakuamini mabadiliko yanayoanza kuonekana kuwa baadhi ya wabunge(makini) wa chama tawala wameanza kuamka akiwemo Waziri Mkuu. Hilo ni somo kwake spika kuwa na yeye pia anatakiwa aanze kubadilika bunge lijali maslahi ya taifa zaidi kuliko ya chama.