Waziri Mkuu akerwa na Kiwanda cha mbolea cha Minjigu kutumia mifuko inayoonesha ni ya Kenya!

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,532
Yaani mbolea izalishwe Tanzania halafu iwe branded Made in Kenya, kweli? Nyie jamaa sasa hizi sifa...Mheshimiwa Rais hawa chapa viboko kabisa!

========

pic+majaliwa.jpg


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema haridhiki na hali aliyoikuta kwenye kiwanda cha kutengeneza mbolea cha Minjingu baada ya kubaini kuwa wanatumia mifuko yenye lebo ya Kenya wakati mbolea hiyo inazalishwa hapa nchini.

Kutokana na hilo, Waziri Mkuu amewataka wamiliki wa kiwanda hicho waandike barua kwa Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli kabla hajamaliza ziara yake Jumatano, Februari 22, 2017 apate nakala ya barua hiyo.

Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Februari 19, 2017) baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo wilaya Babati akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake mkoani Manyara. Waziri Mkuu amerejea Babati leo akitokea Dar es Salaam ambako alikuwa na ratiba za kitaifa.

“Nilikuja kukagua kiwanda baada ya kupokea malalamiko kuwa mbolea hii haikubaliki huko vijijini. Watafiti wameonyesha kuwa ikitumika inasaidia kutoa mazao mengi. Lakini wakati niko kiwandani nimekerwa kukuta mifuko ya kupakia mbolea hii ina anuani ya Nairobi, Kenya wakati mali ghafi inatoka Tanzania,” amesema.

“Ni kwa nini mifuko hii ina anuani ya Kenya? Hapa tulipaswa tuone anuani ya Babati! Je mlipata kibali kutoka serikalini? Tena kuna lebo ya TBS. Kwa nini Tanzania haionekani? Kwani malighafi iko Kenya? Haiwezekani, ni lazima uandike barua na uombe radhi kwa Mheshimiwa Rais Magufuli. Yeye anahimiza ujenzi wa viwanda ndani ya nchi, halafu ninyi mnafanya hivyo?”

Akiwa ndani ya kiwanda hicho, Waziri Mkuu alikuta baadhi ya mifuko ya mbolea ikiwa imeandikwa: ‘County Government of Bungoma’, ina nembo ya Serikali ya Kenya, na anuani ikionesha kuwa mbolea hiyo imetengenezwa na kiwanda cha mbolea cha Minjingu lakini anuani inasomeka P. O Box 2941 – 00200 Nairobi, Kenbro Industrial Park, Mombasa Road; namba ya simu +254-20-6000-970 lakini mifuko hiyo pia ina muhuri wa TBS.

Baadhi ya mifuko ilikuwa ikipakiwa ndani ya lori tayari kwa kusafirishwa kwenda kwa wateja.

Pia amesema atamwagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage aje hapa na wanasheria wake na wataalamu kutoka Tume ya Ushindani wa Kibiashara (FCC) ili waje kuangalia hatua gani zinapaswa kuchukuliwa.

“Kwa staili hii hii tumeona watu wakinunua kahawa yetu na kwenda kuipakia upya huku wakiweka lebo za kwao. Leo hii hata Tanzanite pia inasemwa imetengenzwa India. Hatuwezi kukubali hali hii iendelee,” amesisitiza.

“Tukiruhusu hali hii, watu watajuaje kuwa mbolea hii ambayo ni first class duniani kuwa inapatikana Tanzania? Kiwanda chetu, ardhi yetu, suala la kutangaza nchi yetu kwa kutumia bidhaa zetu litafanikiwa kwa njia hii kweli?”

“Nataka wakati namaliza ziara nipate taarifa ya hili jambo pamoja na nakala ya barua ambayo imetumwa kwa Mheshimiwa Rais,” amesisitiza.

Akitoa maelezo kuhusu hali hiyo, Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Bw. Tosky Hans alimweleza Waziri Mkuu kwamba wametumia lebo hiyo kutokana na makubaliano na wanunuzi jibu ambalo Waziri Mkuu hakulikubali na kusisitiza kuwa anapaswa aombe radhi.

Waziri Mkuu kesho anaendelea na ziara yake wilayani Mbulu ambako atatembelea hospitali ya Haydom, kuzungumza na watumishi wa wilaya hiyo na kuzindua shule ya sekondari Singland.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, FEBRUARI 19, 2017.
 
nimeona hiyo habari kwenye tv jinsi yule mkurugenzi wa kiwanda alivyokuwa anatetemeka kutoa majibu ya kuridhisha kwa PM.

safi sana waziri mkuu majaliwa.hakika hakuna jiwe litakalo salia awamu hii....madhara ya speed ya utawala huu yanaenda mpaka kwa majirani.
 
Majaliwa ana busara sana, ingekua JPM hapo angemtumbua kwanza boss wa Minjingu phosphate then mengine yafuate.

Hongera Majaliwa kwa kuelewa vema maana ya uongozi..
Kamuagiza ajieleze kwa mukulu na ampe nakala,sijui mkulu asipomtumbua huyu ndugu
 
Publicity, soon utasikia.
Half binafsi sioni kazi ya Charles Mwijage zaidi ya kuropoka na kupiga selfie na waekezaji.

Namfananisha sana Mwijage na Aggrey Mwanry enz zake Tamisemi kwa kuropoka ovyo
Hahaa nyuki wa mashineni
 
Mimi kama Mkenya naja kuwaeleza kuwa watu wengi nje ya Afrika hudhania Tanzania ni mkoa wa Kenya. Ndio maana utaskia watu wakisema Mlima Kilimanjaro uko Kenya n,k
 
Mimi kama Mkenya naja kuwaeleza kuwa watu wengi nje ya Afrika hudhania Tanzania ni mkoa wa Kenya. Ndio maana utaskia watu wakisema Mlima Kilimanjaro uko Kenya n,k
Sawa mkenya endelea kuwaambia sie ni mkoa jirani na kericho hapo maana akili zenu mwazijua wenyewe...ila zamu hii mtanyooka EPA tumewaachia viherehere,COW tumeivuruga,EAC federation tunanyaata...mtawadanganya wa nje sie tushawajua nyie hamfurukuti,semeni Magufuli rais wenu pia
 
Labda niulize swali dogo, kwani ikiwekewa label ya Kenya inasafirishwa kwenda Kenya au inauzwa humu Nchini (TANZANIA)?
 
Publicity, soon utasikia.
Half binafsi sioni kazi ya Charles Mwijage zaidi ya kuropoka na kupiga selfie na waekezaji.

Namfananisha sana Mwijage na Aggrey Mwanry enz zake Tamisemi kwa kuropoka ovyo
Ha ha ha mwanry akikujibu utakubali japo unajua ni fix, lilikuwa linaongea kwa uchungu kweli utadhani ni kweli tupu.

Sijui huko mkoani kwake watamdanganya vipi
 
Miye nimeshindwa kuelewa wale wakaguzi wa bidhaa wa Tz hawakuona hilo.Wao hawakagui vifungashio kwani.
Wapiga hela tu, ni sawa na wakaguzi wa madini kwenye mineral site zote. Hakuna kazi wafanyayo.

Hata ukiwauliza kiasi gani kimesafirishwa, hawana jibu
 
Back
Top Bottom